DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com

              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za pole Mkuu wa Mkoa na wananchi wa Mkoa wa Manyara kutokana na maafa makubwa yaliyowapata wachimbaji madini katika machimbo ya Tanzanite ya Mererani, Wilayani Simanjiro, mkoani humo.

 

Rais amepokea kwa masikitiko, huzuni na mshtuko mkubwa taarifa ya janga hilo kubwa.

 

Rais Kikwete amehuzunishwa na upotevu wa maisha ya watu ambao mpaka sasa imethibitika kuwa wamepoteza maisha, yaliyosababishwa na kujaa kwa maji katika mashimo ya machimbo hayo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

 

Rais pia anawaombea wachimbaji ambao taarifa zao hazijathibitika waweze kupatikana haraka wakiwa hai na salama. Rais Kikwete pia anawaombea wote walioumia katika ajali hiyo kupona haraka.

 

Rais anatoa pole kwa familia ambazo zimeathirika na janga hilo na kuzihakikishia kuwa yuko pamoja nao katika wakati huu wa majonzi na huzuni. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu pema peponi.

 

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais na Habari,

Butiama, Mara

Jumapili, 30 Machi 2008.