DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown leo (Jumatano,
Aprili 16, 2008), amemshutumu Rais Robert Mugabe wa
Shutuma hizo za Brown zimetolewa kwenye siku ambako
Uingereza na Marekani, kwa pamoja, zimeongeza kasi ya shinikizo lao kwa
Serikali ya Rais Mugabe kuhusiana na uchaguzi mkuu huo.
Nchi hizo mbili zimetumia nafasi ya mkutano wa
viongozi wakuu ulioitishwa kujadili jinsi Umoja wa Mataifa (UN) unavyoweza
kushirikiana na Umoja wa Afrika (AU), katika kutatua migogoro ya Afrika, kuishambulia
Serikali ya Mugabe ya
Waziri Mkuu Brown amekuwa wa kwanza kuzungumza katika
kikao hicho cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwenye Makao Makuu ya UN
mjini
“Uchaguzi ulioibiwa hauwezi kamwe na kwa njia yoyote
ile kuwa uchaguzi wa kidemokrasia,” amesema Brown katika hotuba yake ya dakika
tano kwenye kikao hicho.
Brown ambaye nchi yake itakuwa Mwenyekiti wa Baraza
la Usalama la UN mwezi ujao, hata hivyo, ametumia hotuba yake hiyo kutoa sifa
kwa Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa juhudi zake katika
kutafuta ufumbuzi wa tatizo la kisiasa la
“Lazima nielezee furaha yangu kwa jitihada
zinazofanywa na SADC kutafuta ufumbuzi wa tatizo la
Naye Mwakilishi wa Kudumu wa Marekani katika UN,
Balozi Zalmay Khalilzad ameishutumu Zimbabwe kwa kusema kuwa ni dhahiri kuwa
wananchi wa Zimbabwe wamenyimwa nafasi ya mabadiliko hata kama walipiga kura
wakitaka kuona mabadiliko katika uongozi na mwelekeo wa nchi yao.
“Ni siku 18 sasa tokea kufanyika kwa uchaguzi mkuu
katika nchi hiyo, na mpaka sasa bado hakuna kauli yoyote juu ya matokeo ya kura
ya urais. Ni dhahiri kuwa wananchi wa
Balozi huyo ametoa mapendekezo matano ya jinsi ya
kutimiza matakwa na utashi wa mabadiliko ya wananchi wa
Waziri Mkuu Brown amekuwa mmoja wa viongozi kadhaa wa
serikali na nchi ambazo wamehudhuria mkutano wa leo uliotishwa na nchi ya
Afrika Kusini ambayo ni mwenyekiti wa sasa wa Baraza la Usalama la UN.
Viongozi wengine ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete,
Waziri Mkuu wa Italia, Romano Prodi; Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo; Rais
wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila; Rais wa Somalia, Abdullahi
Yusuf Ahmed; Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi na Mwenyekiti wa Tume ya AU,
Alpha Omar Konare.
Viongozi na wawakilishi wa nchi 42 wamezungumza
katika kikao cha leo.
Mwisho.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais na Habari
17 Aprili, 2008