DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete: Toeni pesa tumalize migogoro Afrika
Mwenyekiti wa
Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametoa changamoto tatu kwa
Umoja wa Mataifa (UN) katika mahusiano yake na AU, ili kwa pamoja, taasisi hizo
mbili ziweze kufanikiwa katika kutatua migogoro ya Afrika.
Akizungumza leo (Jumatano, Aprili 16, 2008) katika Baraza
la Usalama la UN mjini New York, Marekani, Rais Kikwete amesema kuwa kuna
umuhimu wa taasisi hizo mbili kuweka taratibu wa jinsi AU inavyoweza kuingilia
migogoro ya Afrika bila kusababisha mgongano na UN.
Amesema kuwa kuna wakati AU inaona umuhimu wa
kuingilia haraka na kumaliza tatizo katika nchi ya Afrika na inafanya hivyo,
hata
Pili, Rais Kikwete amesema kuwa upo umuhimu mkubwa wa
UN kuisaidia AU katika kujenga uwezo wake wa kuingilia na kumaliza migogoro ya
Afrika haraka na bila ucheleweshaji wowote.
Pia Rais Kikwete amesema kuwa suala la kuijengea AU
uwezo, hasa linalohusiana na umuhimu wa UN kuruhusu ulinzi wa amani
unaoidhinishwa na UN na kuendeshwa na taasisi za kikanda
Kwa sasa taratibu za UN hairuhusu Umoja huo kugharimia
shughuli hizo, hata
Rais Kikwete ametoa mapendekezo hayo mahsusi wakati
anahutubia kikao maalum cha ngazi ya juu cha pamoja kati ya Baraza la Usalama
la UN na Baraza la Amani na Usalama la AU.
Kikao hicho kinatafuta njia za jinsi taasisi hizo zinavyoweza
kushirikiana katika kutatua migogoro ya kisiasa ya Afrika.
Kikao hicho cha aina yake kimeitishwa na Afrika Kusini
ambayo ndiyo mwenyekiti wa Baraza la Usalama la UN kwa mwezi huu wa Aprili.
Alikuwa ni Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini ambaye alifungua
kikao hicho kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa UN wa masuala ya siasa,
B. Lynn Pascoe kuzungumza na kufuatia na Rais Kikwete.
Miongoni mwa viongozi wengine maarufu waliozungumza
katika kikao hicho ni Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown; Waziri Mkuu wa
Italia, Romano Prodi; Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo; Rais wa DRC, Joseph
Kabila na Rais wa Somalia, Abdullahi Yusuf Ahmed.
Wengine ni Waziri Mkuu wa
Jumla ya viongozi wa serikali na nchi pamoja na
wawakilishi wao kutoka nchi 42 wamezungumza katika kikao hicho maalum.
Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa UN, Ban
Ki Moon aliahidi kuwa UN iko tayari kuendelea kushirikiana na AU katika
kumaliza migogoro inayoendelea katika Bara
Ban Ki Moon amesema kuwa Afrika ni Bara ambalo
limekuwa moyoni mwake hata kabla ya kushika madaraka makubwa ya UN.
Amesema kuwa tokea kukamata madaraka ya ukatibu mkuu,
ametembelea nchi 11 za Bara
Amempongeza na
kumshukuru Mwenyekiti wa Tume ya AU, Konare kwa mchango wake katika AU ambako
amekuwa kiongozi wa kwanza tokea kuanzishwa kwa umoja huo. Konare anamaliza
muda wake mwishoni mwa mwezi huu.
Mwisho.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais na Habari,
17/04/2008