DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
TRL yaahidi kuongeza ufanisi katika kuendesha Reli ya Kati
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imeahidi kuongeza ufanisi wake katika uendeshaji wa
Reli ya Kati, ili kuhakikisha kuwa Reli hiyo
inatoa mchango mkubwa zaidi katika
uchumi wa
Kampuni hiyo imetoa ahadi
hiyo leo, Ijumaa, Januari 16, 2009 wakati uongozi wa TRL ulipokutana na kufanya mazungumzo
na Rais Jakaya
Mrisho Kikwete katika mfululizo wa mikutano yake
na viongozi wa Wizara mbalimbali
na mashirika yake ili kutafakari
utendaji wa Serikali yake.
Mkutano wa leo,
Katika mkutano huo uliofanyika
Ikulu,
TRL ni kampuni
tanzu inayomilikiwa kwa pamoja kati
ya Serikali ya
Kampuni hiyo iliundwa mwaka
juzi, 2007, kwa
ajili ya kuendesha Reli ya Kati baada ya
RITES kuwa imeshinda zabuni ya kuendesha
Reli hiyo ya kati kwa
miaka 25.
Uongozi huyo wa
TRL umetoa ahadi hiyo ya kuongeza
ufanisi baada ya kikao cha leo
kuwa kimejadili hali ya utendaji
ya kampuni hiyo, na matatizo
ambayo yamekuwa yanaikwamisha kampuni hiyo kutoa huduma
bora zaidi kwa wateja.
Baada ya mkutano huo
wa leo kuwa
umejadili masuala mbali mbali ya
Reli hiyo ya Kati ikiwa ni
pamoja na utunzaji wa reli
hiyo, usalama wake, hali yake ya
kifedha na mambo mengine, uongozi wa TRL umeahidi kuongeza ufanisi wake ili kutoa huduma
bora zaidi kwa Watanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16 Januari, 2009