DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Wadau wakubaliana kumaliza msongamano Bandari ya Dar
WADAU wote Wakuu wa Bandari ya
Wadau hao, kila mmoja
wao, amekubali kutoa mchango wake katika kuhakikisha kuwa mlundikano wa mizigo
katika Bandari hiyo unamalizwa ili kuiwezesha Bandari hiyo kufanya
kazi kwa ufanisi zaidi.
Wadau hao wamefikia msimamo
huo katika majadiliano ya kina na ya wazi wakati walipokutana
na Rais Jakaya
Mrisho Kikwete katika mkutano maalum ulioitishwa kujadili na kukubaliana
juu ya njia
za kupunguza ama kumaliza mlundikano
wa bidhaa katika Bandari hiyo.
Mkutano huo uliofanyika leo, Ijumaa,
Januari 16, 2009 Ikulu,
Mkutano huo uliohudhuriwa na Makamu
wa Rais Dk
Ali Mohamed Shein, Waziri wa Miundombinu Dk Shukuru Kawambwa
na Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo umehudhuriwa pia na uongozi
wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na ule wa
Bandari yenyewe ya Dar es Salaam.
Wengine waliohudhuriwa mkutano huo ni Kampuni
ya Kupakua na Kupakia Mizigo
katika Bandari ya Dar Es Salaam (TICTS), Mawakala
wa Kuondoa Mizigo Bandarini (Clearing and
Forwarding Agents), Chama cha Wamiliki Meli Tanzania (Tanzania Shippers Association), Chama cha Wasafirishaji Tanzania (Tanzania Transporters Association) na Chama cha Wamiliki wa Vituo vya
Kontena Nje ya Bandari (ICD,s).
Miongoni mwa hatua ya
kwanza itakayochukuliwa kumaliza
mlundikano huo ni kuondoka
haraka iwezekanavyo kiasi cha makontena 5,332 ya mizigo ambayo
yamelundikana katika Bandari hiyo.
Makontena hayo yatahamishiwa katika ICD’s zenye wa kuchukua
zaidi ya makontena 8,300 kwa wakati mmoja na
ambazo kwa sasa hazina mizigo.
Wadau hao wamekubaliana kuwa moja ya
matatizo makubwa na yanayosababisha
msongamano katika Bandari hiyo ni
baadhi ya waagiza mizigo kuigeuza Bandari ya Dar es Salaam kuwa ghala la kuwekea
mizigo badala ya Bandari hiyo
kuruhusiwa kuwa sehemu ya kupitishia
mizigo tu, iwe ya kusafirisha
nje ya nchi
ama ya kupokelewa
nchini kutoka nje.
Katika mkutano huo pia
imekubaliwa kuchukua hatua za kuzungumza
na nchi
jirani za
Imetolea na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16 Januari, 2009