UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imesema kuwa inatarajia
kuwa mfumuko wa bei uliopanda ghafla mwaka jana, kwa
sababu ya kupanda mno kwa
bei za mafuta
na vyakula (nafaka), utaanza kushuka katika siku za karibuni,
na hivyo kuteremsha gharama za maisha.
BOT imesema kuwa sababu
kubwa ya mfumuko wa
bei kubakia juu kwa sasa,
baada ya bei ya mafuta
kuwa imeshuka, ni gharama kubwa
za usafirishaji wa vyakula.
Mfumuko wa bei nchini ulikuwa asilimia 13.5 kwa mwezi uliopita wa Desemba kutoka
asilimia 8.6, kabla ya kuanza kupanda
ghafla na kwa kiasi kikubwa
kwa bei ya
mafuta na bei duniani na
ile ya chakula.
Pamoja na hali hiyo, BOT inabashiri kuwa lengo la ukuaji
wa uchumi kwa asilimia 7.5 bado linaweza kufikiwa.
Maelezo hayo ya BOT yako
katika ripoti ya benki hiyo
iliyowasilishwa na
Gavana wa Benki Kuu ya
Mkutano huo uliofanyika Ikulu,
Tofauti na mikutano
aliyoifanya mwanzoni mwa utawala wake ambako Rais alitembelea
kila Wizara na kutoa maelekezo
yake, mikutano ya sasa inafanyika
Ikulu kati ya Rais na
viongozi wa juu wa Wizara
mbalimbali na taasisi za Wizara
hizo.
Gavana Ndullu amemwambia Rais Kikwete kuwa
utafiti uliofanyika katika miji yote
nchini kwa
mwaka mzima wa jana, 2008, unaonyesha kuwa mfumuko wa bei
ulishuka kwa bidhaa na huduma
zote zisizokuwa chakula.
Utafiti huo wa
BOT unaonyesha kuwa mfumuko wa bei
wa chakula uliongezeka kutoka asilimia 10.1 Januari mwaka jana hadi
kufikia asilimia 18.6 mwezi uliopita wa Desemba, mwaka
jana.
Amesema Gavana Ndullu: “Hata hivyo, kutokana
na mwenendo
wa hivi karibuni
wa bei za
mafuta katika soko la dunia, ambapo bei ya
mafuta imeshuka kiasi kikubwa, mfumuko wa bei
unatarajiwa kuanza kushuka katika siku za usoni.”
Gavana pia amesema kuwa
kumekuwapo na
kasi kubwa ya ongezeko la mikopo kwa sekta
binafsi kutoka mabenki katika kipindi cha miezi mitano ya mwanzo
ya mwaka wa fedha 2008/2009.
Amesema kuwa mikopo hiyo
imeongezeka kwa
kiasi cha sh. bilioni 840.4
ambalo ni ongezeko la asilimia 85 ya ongezeko la sh bilioni 900 zilizokusudiwa kukopesha sekta binafsi kwa
mwaka mzima.
Gavana Ndullu pia ameeleza
kuwa hazina ya fedha za
kigeni katika BOT hadi kufikia Desemba
mwaka jana
ilikuwa ni dola za Marekani
bilioni 2,894.42, ambazo zinatosha kuweza kuagiza bidhaa kutoka nje kwa
kipindi cha miezi minne 4.3.
Kuhusu sekta ya fedha,
Gavana amesema kuwa sekta hiyo
imeendelea kuimarika mwaka uliopita na kuwa mabenki 31 kati ya mabenki 34 yanayofanya
kazi nchini yanakidhi kiwango cha mtaji unaoweza kuhimili madai (capital adequacy
ratio) kwa asilimia inayofikia asilimia 17, ikilinganishwa na kiwango kinachokubaliwa kimataifa, yaani asilimia 10.
Gavana amesema kuwa kwa jumla mabenki yote nchini
yanayo ukwasi (capital) wa kutosheleza malipo kwa wateja
wao kwa kiwango
cha asilimia 50.7 ikilinganishwa
na kiwango kinachokubaliwa kibenki cha asilimia 20.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
19
Januari, 2009