DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mwenyekiti wa Umoja
wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini asubuhi ya leo, Jumamosi,
Januari 31, 2009, kwenda
Mkutano huo wa 12
utafanyika kwa siku mbili kuanzia keshokutwa, Jumatatu, Januari 2, 2009, kwenye
Ukumbi wa UNCC-EAC mjini
Mkutano huo
utatanguliwa na Kikao Maalum cha wakuu hao wa nchi wanachama wa AU
kitakachofanyika kesho, Jumapili, Februari Mosi, 2009, kujadili maendeleo ya
kuanzishwa kwa Serikali ya Umoja wa Afrika.
Kikao hicho maalum
kitafanyika chini ya uenyekiti wa Rais Kikwete, katika nafasi yake kama
Mwenyekiti wa AU, na ni mwendelezo wa majadiliano ya suala hilo kama
ilivyoamuliwa katika kikao kilichopita cha AU kilichofanyika Sharm El Sheikh,
Misri, Juni, mwaka jana.
Kikao hicho maalum
kitapokea na kujadili ripoti ya Kamisheni ya AU juu ya mapendekezo ya jinsi ya
kuanzishwa kwa Serikali hiyo.
Kikao hicho
kitafuatiwa na Mkutano wenyewe wa 12 wa wakuu wa nchi hizo utakaofanyika kwenye
ukumbi huo huo wa UNCC-ECA.
Rais Kikwete
ataufungua Mkutano huo ambao pia utamchagua mwenyekiti mpya wa AU, ambaye
atachukua nafasi ya Rais Kikwete, anayemaliza muda wake kwenye nafasi hiyo.
Miongoni mwa
wazungumzaji kwenye ufunguzi huo, mbali na Rais Kikwete mwenyewe, watakuwa ni
pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Ato
Meles Zenawi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Jean Ping, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki-Moon, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu (Arab League)
Amr Moussa.
Kwenye siku ya pili
ya Mkutano huo, Jumanne, Februari 3, 2009, wakuu hao watajadili zahama ya
kifedha inayoikabili dunia baada ya kuwa wamewasikiliza wataalam mbalimbali wa
masuala ya fedha katika Afrika na duniani.
Kwenye siku hiyo ya
pili na ya mwisho ya Mkutano huo,
Mbali na mkutano
huo, Rais Kikwete pia atahudhuria Mkutano wa 20 wa Kamati ya Utekelezaji ya
Wakuu wa Nchi za NEPAD uliopangwa kuanza asubuhi la leo, Jumamosi, Januari 31,
2009.
Baadaye mchana,
Rais Kikwete atahudhuria mkutano maalum wa eneo la Maziwa Makuu ambao utapokea
na kujadili ripoti kuhusu hali ilivyo katika Mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Ripoti hiyo
itawasilishwa na marais wa zamani, Olusegun Obasanjo wa Nigeria na Benjamin
Mkapa wa Tanzania ambao wameombwa na Umoja wa Mataifa na Wakuu wa Nchi za
Maziwa Makuu kuongoza jitihada za kuleta amani Mashariki mwa DRC.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
31 Januari, 2009