DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU
ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mzee
Chediel Mgonja kilichotokea tarehe 30 Januari, 2009 katika Hospitali ya Jeshi
la Wananchi wa
Nilimfahamu Ndugu Mgonja wakati akiwa
katika Utumishi wa Umma,
akiwa Waziri wa Serikali katika
Wizara mbalimbali zikiwamo Wizara ya Mambo ya Nje,
na pia Wizara
ya Elimu.
Alikuwa ni mtumishi hodari, mahiri, mwaminifu na mwadilifu.
Amechangia maendeleo ya nchi yetu
katika nafasi hizo mbalimbali na tutaendelea
kukumbuka mchango wake huo muhimu katika
uhai wa taifa
letu.
Naungana nanyi katika wakati huu
mgumu na
wa majonzi makubwa kutokana na msiba mkubwa
uliowakuta. Tunaelewa machungu mliyonayo kutokana na kuondokewa
na mpendwa wenu na kiongozi
wa familia. Lakini ni kazi ya Mungu na
haina makosa.
Tunawatakia mazishi mema na kuwaombeeni
kwa Mungu muwe na nguvu
ya kutosha kuweza kuvumilia majonzi ya msiba
huu . Tuzidi kumuombea marehemu,
apate mapumziko mema. Amin.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
31 Januari, 2009