DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Na
Mwandishi Maalum,
MAELFU
ya wakulima wadogo nchini wanatarajiwa kunufaika na mpango wa uwezeshaji,
ambako kila mkulima atakopeshwa mahitaji ya kilimo yenye thamani ya zaidi ya sh
200,000 kwa mwaka, ili kumwezesha kuinua uzalishaji na kujiongezea kipato.
Chini
ya mpango huo unaogharimiwa kwa pamoja na taasisi mbalimbali duniani, ikiwamo
ile ya Bill and Melinda Gates Foundation, wakulima hao watapewa mbegu, mbolea
na mahitaji mengine ya kuwezesha kuinua kiwango cha uzalishaji. Wakulima pia watahakikishiwa soko la mazao
Ujumbe
wa watu 17 kutoka taasisi hizo umemwambia Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumatatu, Februari 9, 2009, kwamba mpango huo utawashirikisha wakulima kiasi
cha 250,000 wa Tanzania katika awamu ya kwanza ya miaka mitatu.
Mbali
na Bill and Melinda Gates Foundation, taasisi nyingine zinazoshiriki katika
mpango na ambao wajumbe wake wamekutana na Rais Kikwete leo, Ikulu, Dar es
Salaam ni Alliance for a Green Revolution in Afrika (AGRA), Standard Bank na
Export Trading Group.
Wakati
wa mazungumzo yake na ujumbe huo, Rais Kikwete ameziomba taasisi zinazoshiriki
katika mpango huo kuongeza idadi ya wakulima wa
Rais
amesema kuwa mpango huo ni muhimu
Rais
ameshukuru na kusema kuwa katika mazingira ambamo asilimia 80 ya wananchi wote
wa
Amesema
kuwa matatizo makubwa ya kilimo cha
“Sisi
hapa bado tunatumia kilo nane za mbolea kwa eka moja wakati wenzetu kule Uholanzi
wanatumia kilo 500, na hivyo siyo jambo la kushangaza kwamba uzalishaji wetu ni
duni na wa chini mno,” Rais Kikwete ameuambia ujumbe huo.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
09 Februari, 2009