UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete leo mchana
katika Ikulu ya Dar-Es-Salaam amempokea na kufanya mazungumzo
na Rais wa
Muungano wa Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Ahmed Abdallah Sambi.
“Nimekuja kukushukuru wewe binafsi na
Tanzania kwa mchango mkubwa mliotoa kwa nchi yangu
ya Comoro, Comoro sasa imekuwa nchi zaidi,
yenye amani na inayoendelea, naomba uendelee na moyo huo
huo” Rais Sambi amemwambia Rais Kikwete.
Rais
Sambi pia amemwomba Rais
Kikwete aendelee kumsaidia na kumpa
ushirikiano zaid Rais mpya aliyechaguliwa
tarehe 26 Disemba, 2010, kufuatia uchaguzi mkuu visiwani humo
ambao kwa mara ya kwanza, uchaguzi huo ulihusisha uchaguzi wa Rais
wa Muungano wa Visiwa hivyo
na pia wa
magavana wa Visiwa vya Ngadzija,
Anjouan na Moheli.
Rais
Kikwete amempongeza Rais Sambi kwa kuongoza uchaguzi huo uliofanyika
kwa amani na utulivu na
kumhakikishia kuwa Tanzania
itaendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi wa visiwa
hivyo. Katika uchaguzi huo wa Disemba 26, 2010 Dkt. Ikililou Dhoinine
aliibuka mshindi.
Wakati
huo huo Rais
Kikwete ameelekea Mkoani Iringa jioni
hii kwa ajili
ya kushiriki maziko ya mama Mzazi wa Mheshimiwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Bibi Tulakela Milia Samnyuha yatakayofanyika
kijijini kwao Yakobi wilayani Njombe kesho Mei 8, 2011.
Mara baada ya kupata
taarifa za kifo cha mama mzazi wa Spika, kilichotokea
tarehe 5 Mei, 2011, Rais Kikwete alimtumia salamu za pole Mhe. Spika kwa niaba yake, familia yake
na Watanzania kwa ujumla na
kumuombea mapumziko mema marehemu Bibi
Samnyuha.
Mara baada ya maziko
hayo Rais Kikwete ataelekea Dodoma kwa ajili ya
kuhudhuria Semina Elekezi kwa ajili ya Mawaziri
na Viongozi Waandamizi wa Serikali
itakayoanzaJumatatu tarehe
9 Mei, 2011.
Mwisho
Imetolewa
na Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari
wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
7
Mei, 2011