PRESS SECRETARY TO THE PRESIDENT
Fax. No. 255-22 2113425
The State House,
Tel:
DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
MSIFANYE KAZI KWA
MAZOEA-KIKWETE
·
Awataka viongozi kuwa
wabunifu
·
Awataka kuachana na ofisi
zao na kwenda kwa wananchi
Na
Maura Mwingira
SERENGETI
14/8/2006
Rais Jakaya Kikwete amewataka viongozi wote katika ngazi za
utendaji na utawala kuachana na tabia ya
kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawe na mawazo mapya yatakayosukuma
maendeleo ya wananchi.
Rais ametoa rai hiyo
jana wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa mkoa wa Mara wakati
alipokuwa akitoa majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku sita Mkoani hapa. Majumuisho
hayo yalifanyika katika hoteli ya Kitalii ya Grument wilayani Serengeti
“Viongozi
tusifanya kazi
Na
kuongeza kuwa ni jambo jema kwa viongozi kutowakemea au kuwakwepa, watu
wanaowaletea mawazo mapya kwa kisingizo cha zamani tulikuwa tunafanya hivi, au
kuwahoji wameyatoa wapi mawazo hayo.
Rais
Kikwete alitoa mfano kwa kusema kuwa hata uteuzi wa wakuu wa wilaya ambao
ulifanyika hivi karibuni haukuwa na mabadiliko makubwa kwa wakuu wa wilaya wa
zamani, karibu nusu yao walibaki na
kuhamishwa vituo vyao vya kazi ili hali 10 wakibakishwa katika vituo vyao vya zamani
kwa sababu mbalimbali zikiwamo za kukaribia kustaafu.
“Tulifanya
hivyo kwa sababu tunataka viongozi hawa waende katika eneo jipya ili wakawe na
mawazo mapya”
Hata
hivyo alibainisha kuwa viongozi hao wa zamani wanaweza kuendelea na staili zao
za zamani, lakini wakatenda kwa kasi
mpya, ari mpya na nguvu mpya, huku wakiwa wabunifu wa mambo mapya.
“Usiwe
kiongozi ambaye ukiamka asubuhi unakwenda ofisini, unasoma mafaili, unauliza kuna
barua ngapi, unasoma magazeti kisha huyo unafunga ofisi, siku imekwisha unarudi
nyumbani” alisema
Na
kuwataka viongozi wajiulize kwa uwazi
ndani ya mioyo
“Jiulize
hivi miye Kikwete baadaya ya uongozi
wangu nataka nikumbukwe kwa lipi, ukijiuliza hivyo ndani ya moyo wako basi
wakati wote unakuwa na jambo jipya. Tukiwa na moyo huu hata kasi ya maendeleo
yetu itakuwa kubwa, lakini tukifanya kazi kwa mazoea hatufiki mbali na hiyo
ndiyo sura ya uongozi” alisisitiza.
Katika
majumisho hayo ambayo yaliwahusisha viongozi wa serikali na chama tawala, Rais Kikwete aliwataka pia kufanya kazi kwa
malengo yanayopimika.
Aliwataka
pia kuwatembelea wananchi katika maeneo wanayoishi na kufanya kazi, kwa kuwa
kwa kufanya hivyo si tu kutawajengea uwezo wa kuyafamu maeneo
“Acheni
kukaa kwenye ofisi zenu kubwa, viti vya kuzunguka na viyoyozi,mkurugenzi wa
halmashauri unatumia muda mwingi kukaa ofisini, na matokeo yake unadanganywa
na maofisa wako, wanajaza night na
kwenda safari kwa kazi ambazo hawakuzifanya. Na matokeo yake wakurugenzi wengi mnapata matatizo kwa sababu
hamko makini” alifafanua.
Rais
alisema kuwa wakurugenzi wengi ni warasimu wakubwa na wanaodhani kuwa heshima
kubwa kwao ni kukaa ofisi kwao. Wanasubiri hadi Mkuu wa Mkoa au Rais afanya
ziara ndipo na wao wanatokea.
“Jamani viongozi tuwe wepesi wa kutatua matatizo ya
wananchi, tuwajali, tusikilize kero zao, na mara nyingi kero nyingi
zinazotolewa na wananchi ufumbuzi wake umo
ndani yenu, vinginevyo wananchi hao wakiyafikisha kwa Rais munaanza oho
majungu, oh watu wafitini, badilizi staili zenu za kufanya kazi, kwa sababu
watu wa nchini wanateseka
Na kwa sababu hiyo aliwataka wakurugenzi wa halmashauri za
miji kuwa macho na masikio
Akasisitiza kuwa kwakiongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa mtaji wao ni
wananchi na si vinginevyo.
Aidha Rais aliwataka viongozi hao kuimarisha utawala bora
kwa kuwa heshima ya serikali ni kutenda
vema.
“Fanyeni vizuri katika utawala, ongozeni vizuri katika
uchumi, simamieni ulinzi na usalama, zingatieni maadili ya kazi na utumishi.
Maana heshima ya serikali ni kuzingatia maadili, kujali taratibu za kazi ,
kuheshimu sheria na kuheshimu haki za binadamu”.
Rais aliwaambia viongozi hao kuwa katika ziara yake hiyo
yako mambo mengi mazuri aliyojifunza. Miongoni mwa hayo ni kwamba wananchi wa
mkoa wa Mara wana ari kubwa ya kujiletea maendeleo
Karibu
wilaya zote au zimekamilisha ujenzi wa shule za sekondari katika kila kata, na
ama nyingine ziko katika hatua za ukamilishaji.
Rais
alisema amegundua pia kwamba mkoa huo una ardhi nzuri inayofaa kwa kilimo
katika baadhi ya wilaya, inazo raslimali za utalii na madini, na kuna ari ya
viongozi katika kuleta maendelo ya kukuza
uchumi wa mkoa huo..
Aidha Rais
alizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili viongozi wa mkoa huo, kuwa ni
pamoja na kupambana na umaskini.
Alisema
kuwa kielelezo kikubwa cha hali ya umaskini wa wakazi wa mkoa huo ni hali ya
nyumba zao, ambazo alisema hazifanani na utajiri mkubwa uliomo mkoani humo
ukiwamo wa ng’ombe.
Na kwa sababu hiyo aliwataka kupambana na mila
zinazokinzana na dhana nzima ya maendeleo, kuwapatia elimu watoto wa kike,
kuongeza kasi katika ukusanyaji wa mapato, kukabiliana na vitendo vya uhalifu, mauaji
ya watu, wizi wa mifugo, uharamia kwenye ziwa, kupambana na magendo ya uuzaji
wa chakula na mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi na kilimo cha bangi.
Alisema kuwa serikali imejipanga vema katika utekelezaji na
kuyapatia ufumbuzi baadhi ya matatizo sugu yanaoukabili mkoa huo, hususani
upatikanaji wa maji
Katika hatua nyingine Rais Jakaya Kikwete amesema yeye
binafsi na kwa kushirikiana na Mkewe Mama Salma Kikwete watafuta wahisani
watakao saidia ujenzi wa mabweni ya kulala wanafunzi wa shule ya sekondari ya
Natta iliyoko wilayani Serengeti.
Rais alitoa ahadi hiyo mara baada ya kufungua bweni la
wasichana lenye uwezo wa kulaza wanafunzi
wa kike 48. Bweni ambalo limepewa jina la Mama Salma Kikwete.
Rais alisema kuwa watajadiliana na mke wake namna ya
kuwapata wafadhili hao ambao alisema kuwa baadhi yake ni marafiki zao, ili
kuwawezesha watoto hasa wa kike kwa
kuanzia na baadaye wa kiume ili wapate malazi yanayoeleweka shuleni hapo.
Shule hiyo imejengwa kwa ushirikiano wa wananchi wa
eneo hili, halmashauri, wadau mbalimbali
akiwamo mbunge wa jimbo
“Nitakwenda kumweleza mke wangu, kwamba kuna bweni huko
limepewa jina lako, lakini si wanafunzi wote wa kike wamepata mahali pa kulala
hivyo atafute njia ya kufanikisha ujenzi kwa ajili ya wanafunzi waliobakia.
Lakini nitamwambia yeye si mama wa wanafunzi wa kike peke yake, bali hata wa kiume
ni mama
Kuhusu ombi la kuipatisha shule hiyo umeme, Rais alisema
kuwa atakwenda kuzungumza na Waziri wa Nishati na Madini kuangalia uwezekano wa
kutenga fedha kutoka fungu la umeme vijiji ili kuiwezesha shule hiyo kupata
umeme.
Jumla
ya shilingi milioni 48 zinahitaji kuvuta umeme na kuupeleka shuleni hapo. Umeme
wa gridi ya taifa unapita karibu kabisa na shule hiyo, lakini unahitajika kubadilishwa
nguvu zake ili uweze kutumika shuleni hapo.
Rais
amerejea jijini Dare s Salaam leo baada ya kumaliza ziara yake mkoani hapa.
mwisho