UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Servacius Beda Likwelile kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Fedha na Uchumi, taarifa iliyotolea Ikulu, Dar es Salaam, leo, Alhamisi, Mei 20, 2010, imeeleza.

 

          Taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon L. Luhanjo imesema kuwa uteuzi huo ulianza Mei 10, mwaka huu, 2010.

         

Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Likwelile alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

 

          Dkt. Likwelile anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Philip Mpango aliyeteuliwa karibuni kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango.

 

Imetolewa na:

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

 

20 Mei, 2010