UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni maalum
katika mjadala wa kimataifa kuhusu
Visheni Mpya ya Kilimo katika
Afrika (Achieving Africa’s New Vision for
Agriculture) utakaofanyika mjini
Cape Town, Afrika
Kusini, kesho, Jumatano, Mei 4, 2011.
Rais Kikwete pia atatembelea
Kituo cha Kimataifa cha Biashara (World Trade Centre) mjini
humo humo kuona maandalizi yanayofanywa kwa
ajili ya kuanzisha kituo kama hicho nchini
Tanzania.
Aidha, kesho hiyo hiyo,
Rais Kikwete atashiriki katika mjadala maalum wa maandalizi
ya kuanzishwa kwa Soko la Mazao
nchini (Commodity Exchange) ambalo
maandalizi yake yanafanywa kwa pamoja kati ya
Serikali ya Tanzania na Benki ya
Dunia (WB).
Rais Kikwete atashiriki katika shughuli hizo muhimu kwa uchumi na maendeleo ya
Tanzania ikiwa sehemu ya ushiriki wake katika Mkutano wa Uchumi Duniani
– Kanda ya Afrika (World
Economic Forum-Africa) unaofanyika mjini Cape Town, Afrika Kusini.
Mwaka jana, mkutano
huo ulifanyika mjini Dar es Salaam, ikiwa ni mara
ya kwanza kwa mkutano huo kufanyika
nje ya mji
wa Cape Town katika historia yake.
Rais Kikwete ameondoka nchini leo,
Jumanne, Mei 3, 2011, kwenda
Cape Town kwa ajili ya mkutano huo
wa siku mbili
ambako pia atashiriki katika shughuli nyingine tatu kuhusu uchumi
na maendeleo.
Washiriki wengine wa
mkutano wa Visheni Mpya ya
Kilimo katika Afrika, ambako Rais Kikwete atakuwa
mgeni maalum, ni pamoja na
viongozi mbalimbali duniani wa serikali,
biashara na uchumi, mashirika ya kimataifa, mashirika
yasiyokuwa ya kimataifa, wasomi na vyama vya
wakulima duniani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
03
Mei, 2011