UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax:
255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Na
MwandishiMaalum, Cape Town, AfrikaKusini
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amesema kuwa uongozi wake hauna muda tena wa
kupoteza katika kuhakikisha kuwa wakulima wa Tanzania wanainuliwa kutoka kwenye umasikini kwa kuhakikisha kuwa kilimo cha Tanzania kinaboreshwa haraka iwezekanavyo.
“Wangu ni uongozi
usiokuwa na muda wa kupoteza. Nina haraka. Sina muda
tena wakusubiri. Tunahitaji kuongeza kasi ya
mapambano ya kuwatoa wakulima wetu katika umasikini.
Watu wetu wameishi katika umasikini kwa
miaka mingi kupita kiasi. Watu
wetu wameteseka sana,” Rais Kikwete
amesema leo,
Jumatano, Mei 4, 2011.
Rais Kikwete ameyasema hayo wakati anashiriki
katika kikao maalum cha kujadili jinsi ya kuanzisha
Soko la Mazaola Tanzania
(Tanzania Commodity Exchange) ikiwani sehemu ya Mkutano
wa 21 wa
Mkutano wa Uchumi Duniani, Kanda ya Afrika, unaofanyika
kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mjini Cape Town, AfrikaKusini.
Mkutano huo ambao mwaka
jana ulifanyika
mjini Dar es Salaam, ikiwa ni mara
ya kwanza kufanyika nje ya Jiji
la Cape Town, umeanza leo mchana na mada
kuu ya mkutano
wa mwaka huu ni Nafasi
ya Afrika katika Mazingira Halisi Mapya Duniani
(Africa’s Role in the New Reality).
Akifunga kikao hicho kuhusu
uanzishwaji wa Soko la Mazao katika
Tanzania, Rais Kikwete amewaambia washiriki kuwa wakati umefika
wa kukabiliana na umasikini ana
kwa ana kwa
nia ya kuupunguza
na hatimaye kuumaliza kabisa kwasababu wananchi wameishi katika maisha ya shida
na dhiki kwa miaka mingi
sana.
Washiriki wa kikao
hicho walijadili uanzishwaji wa Soko hilo baada
ya mawasilisho yaliyofanywa na mtaalamu wa masoko
ya mazao, Bwana Barat. Katika mawasilisho yake,
Bwana Barat ameeleza jinsi soko la mazao la Ethiopia alilosaidia kuanzisha katika miaka ya
karibuni linavyoshamiri.
Bwana Barat pia
ametoa maelezo ya jumla ya
jinsi soko la mazao linavyotakiwa kufanya kazi, nani
analimiki, nani analidhamini, nani anatoa fedha za
uanzishwaji wake, nani wanashiriki katika shughuli zake, nani ananufaika nalo na kwa kiasi gani.
Aidha, Bwana Barat ameeleza muundo anaoupendekeza kwa
ajili ya Soko la Mazao la Tanzania ambalo anapendekeza kuwa lianzeshughuli zake kabla ya
mwisho wa mwaka huu.
Bwana Barat amesema
kuwa moja ya malengo makuu
ya soko hilo
litakuwa ni kuwageuza wakulima wa Tanzania kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuwafanya
wajasiria mali katika kilimo ili
waweze kunufaika kwa kiasi kinachostahili
na jasho lao.
Mwisho.
Imetolewa na:
Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais,
Safarini,
Cape
Town, Afrika Kusini
05
Mei, 2011