UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA MHARIRI WA GAZETI LA UHURU
Waziri Mkuu
wa India, Mheshimiwa Manmohan Singh amekubali mwaliko wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kutembelea Tanzania wiki ijayo.
Mheshimiwa Singh amekubali
mwaliko huo katika barua yake
aliyomwandikia Rais Kikwete na
iliyokabidhiwa kwake na Balozi wa
India katika Tanzania, Mheshimiwa
K.V. Bhagirah wakati Balozi huyo alipokutana
na kufanya mazungumzo na Rais
Kikwete leo, Alhamisi, Mei 19, 2011, Ikulu,
Dar es Salaam.
Kwa mujibu
wa mwaliko
wa Rais Kikwete
uliokubaliwa na Mheshimiwa Manmohan Singh, Waziri Mkuu huyo
wa India atakuwa nchini kwa siku
mbili za ziara rasmi kuanzia
Mei 26.
Katika barua
yake kwa
Rais Kikwete, Mheshimiwa Singh amesema: “Nakushukuru kwa barua ya kunilialika
kuitembelea nchi yako nzuri. Itakuwa ni
heshima kwangu kuitembelea Tanzania na naukubali mwaliko huo kwa furaha
kubwa.”
Ameongeza Waziri
Mkuu huyo: “Nina ari kubwa kukutana
nawe na
marafiki wengine wa Tanzania wakati wa ziara hiyo
na kujadili njia ya kuuinua
uhusiano kati ya nchi zetu
kwenye ngazi mpya kwa manufaa
ya wananchi wa nchi zetu
mbili.”
Kabla ya kuja Tanzania, Mheshimiwa Singh atahudhuria Mkutano wa Pili kati ya India na
Afrika utakaofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambako
Bara la Afrika litawakilishwa
na wakuu wa jumuia za
uchumi za Afrika.
Mkutano wa kwanza kati ya India na Afrika
uliofanyika mwaka 2008 ulikuwa chini ya
uenyekiti wenza wa Rais Kikwete
na Waziri Mkuu Singh na ulifungua
ukusara mpya katika mahusiano kati ya pande
hizo mbili. Wakati huo, Rais
Kikwete alikuwa Mwenyekiti wa
Umoja wa Afrika (AU).
Tanzania
na India zimekuwa
na uhusiano wa kihistoria ambako
viongozi wa juu wa nchi
hizo zimefanya ziara za kubadilishana
na biashara kati ya nchi
hizo mbili imefikia thamani ya dola za
Marekani bilioni 1.1. Uwekezaji wa
makampuni ya India katika uchumi wa
Tanzania unakadiriwa kufikia
kiasi cha dola za Marekani bilioni
1.3.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
19
Mei, 2011