UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Misaada ya Kimataifa ya
Maendeleo wa Uingereza, Mheshimiwa Andrew Mitchel kuhusu fedha ambazo Serikali
ya Tanzania inadai ilipwe na kampuni ya kuuza silaha ya nchi hiyo ya British
Aerospace (BAE).
Katika mazungumzo hayo kwenye
Ukumbi wa Palace of Conferences katika kijiji cha Sipopo, nje kidogo ya mji
mkuu wa Equatorial Guinea katika Kisiwa cha Bioko, viongozi hao wawili
wamekubaliana kuendelea na jitihada za kuishawishi BAE kuilipa Tanzania fedha
hizo ambazo ni haki yake.
Tanzania inadai kulipwa fedha
zake kiasi cha paundi za Uingereza milioni 29.5 zinazotokana na Tanzania
kutozwa kiasi kikubwa zaidi kuliko kile kilichotakiwa kulipwa wakati inanunua
rada kutoka BAE.
Ununuzi wa rada hiyo
ulisababisha matatizo makubwa yakiwemo madai ya rushwa na hatimaye kampuni hiyo
ya BAE ilifikishwa mahakamani kwa madai hayo ya kutoa rushwa katika ununuzi wa
rada hiyo.
Hatimaye mahakama iliamua kuwa
BAE haikutoa rushwa isipokuwa kuwa ilifanya makosa katika vitabu vyake vya
mahesabu lakini kampuni ikaamuliwa pia kulipa kiasi cha paundi milioni 29.5
kuirudishia Tanzania ambayo ni fedha yake kihalali kwa sababu ilidhulumiwa
fedha zake.
Hata hivyo, kampuni hiyo pamoja
na kuamuliwa kuilipa Tanzania moja kwa moja, iliamua kutoa fedha hizo kwa
taasisi isiyokuwa ya kiserikali ambayo ndiyo ingeleta fedha hizo Tanzania kwa
njia ya kutoa huduma.
Tanzania imepinga hatua hiyo na
majuzi ilitoa taarifa kali Bungeni kupinga hatua hiyo ya BEA, Serikali inataka
kuziingiza fedha hizo katika kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kununua vitabu
kwa ajili ya wanafunzi na kujenga madarasa na nyumba za walimu.
Viongozi hao wawili pia
wamezungumzia hali ilivyo katika Libya ambako Rais Kikwete amemwelezea
Mheshimiwa Mitchel maoni ya viongozi wa waafrika kuhusu kampeni ya kuipiga
mabomu inayoendeshwa na majeshi la Umoja wa Kujihami wa Ulaya (NATO) dhidi ya
Libya.
Imetolewa
na:
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
Safarini,
Malabo,
Equatorial Guinea.
01 Julai, 2011