PRESS SECRETARY TO THE PRESIDENT
Fax. No.
255-22 2113425 The State House,
Tel:
DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Na
Mwandishi maalum
22/9/2006
NewYork
Tanzania ni moja
kati ya nchi tano zitakazonufaika na msaada wa Dola za Kimarekani milioni 250
zitakazo tolewa kupitia Mpango wa Rais Billi Clinton
unaoshughulikia matatizo mbalimbali yanayoikabili dunia hususani nchi
zinazoendelea, maarufu kama Clinton Global Initiative (CGI).
Rais Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton ambaye ndiye mmiliki
wa mpango huo, alitangaza mbele ya Rais Jakaya Kikwete na viongozi
mbalimbali wa serikali, mashirika mkubwa na biashara na taasisi zisizo za
kiserikali, kwamba Tanzania ni nchi mojawapo itakayonufaika na fedha
hizo.
Aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka
wa siku tatu wa taasisi yake, ulioanza juzi hapa NewYork ,
Marekani.
Rais huyo Mstaafu wa Marekani, alisema kuwa fedha hizo ambazo
zimetolewa na Bangladesh Royal Advancement Committee (BRAC), kama mchango
wake kwa taasisi yake, zitaelekezwa katika uendelezaji wa sekta ya
kilimo, upatikanaji wa huduma za afya na udhibiti wa malaria, uendelezaji
wa elimu, kukuza ujasiriamali kwa kupitia mipango endelevu ya huduma za
fedha.
Nchi nyingine zitakazonufaika na fedha hizo ni
Katika mkutano huu wa siku
tatu wa taasisi hiyo ya Bill Clinton, ambao pia ulihudhuriwa na Mke wa
Rais wa Marekani Laura Bush na kutangaza mikakati ya upatikani wa maji safi na
salama kwa nchi za Afrika.
Wajumbe wa mkutano huo
ambao walipata muda wa kujadiliana na kubadilishana
mawazo kuhusu kuhusu mada kuu nne zilizowasilishwa kwa nyakati tofauti mbele
yao .
Mada hizo ni pamoja na mabadiliko ya hali ya
hewa na uhifadhi wa mazingira, afya, maji safi na maji taka,
upunguzaji wa umaskini, na tofauti za mitazamo ya kidini.
Rais Jakaya Kikwete
alishirikia katika mjadala uliozungumzia afya, upatikanaji wa maji
Akitoa mchango wa mawazo yake
kuhusu mada hiyo, Rais Jakaya Kikwete alisema kwamba, suala la upatikanaji wa
maji
Aliwaeleza wajumbe waliokuwa wakiijadili mada hiyo, kwamba
serikali ya
Alisema kuwa changamoto kubwa kwa serikali yake iko katika
upatikanaji wa raslimali kwa maana ya fedha na rasilimali watu.
Rais Kikwete alibainisha kwamba, upatikanaji wa raslimali za kutekeleza
mikakati ya kuwapatia Watanzania maji
Alitoa mfano kuwa wanawake na watoto wa kike ndio ambao wakitumia
muda wao mwingi katika kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
“Tatizo letu sisi haliko katika mpango mkakati na sera, hivyo
vyote tunavyo, kinachotukwamisha ni uwezo wa kifedha na kimtaji wa kukabiliana
na changamoto hiyo, na ndio maana tumekuwa tukiomba nchi wahisani na wadau wa
maendeleo watusaidie.
Alisema kuwa ikiwa uwekezaji katika sekta hiyo utakuwa ni
mkubwa ni wazi kwamba utatoa nafuu kubwa kwa wanawake na watoto wa kike ambao
wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta maji.
Aidha Rais Kikwete alisema kuwa utolewaji wa elimu kuhusu matumizi
bora na endelevu ya maji inahitajika.
Rais Kikwete alifafanua kwamba, ni jambo lisilo na mjadala kwamba,
lazima kuwapo na ushirikiano miongoni mwa wadau wote wanaotumia raslimali maji,
yaani wale wanaoitumia raslimali hiyo kwa matumizi ya majumbani na wale
wanaotumia kwa kilimo.
Alibainisha kwamba moja ya changamoto kubwa inayoikabili
serikali yake na nchi zinazoendelea kwa ujumla ni katika kuwashawishi nchi
wahisani na wafadhili kuwekeza katika sekta ya maji.
Alisema kuwa wadau wengi wa maendeleo wamekuwa wakikazania
kuwekeza katika sekta za afya, elimu na miundombinu na kusahau au kutoipa
umuhimu wa pekee sekta ya maji.
Alisema kuwa changamoto kubwa zinazozikabili nchi zinazoendelea,
Tanzania ikiwamo, ni ukosefu wa mitaji, na raslimali watu inayoweza kutoa
mchango wa kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji safi, salama na uhifadhi wa
maji taka.
Nao washiriki wengine wa mjadala huo wa afya, maji safi na salama
na maji taka, walibainisha kwamba huu ni wakati muafaka kwa wadau mbalimbali,
wakiwamo viongozi wa seriakali ya Marekani na mashirika makubwa ya biashara kukubali
kubadilika kimawazo na kuwekeza katika sekta ya maji,
Washiriki wa mdahalo huo, walibainisha umuhimu wa sekta ya umma na
sekta binafsi kushirikiana katika kulitafutia ufumbuzi tatizo la uhaba wa
maji safi na salama, kwa nchi
zinazoendelea.
Walionya kwamba kutokana na taarifa mbalimbali za utafiti, kuwa
vita kuu ya dunia inayoweza kutokea haitahusu kugombea mafuta bali itahusu
vita vya kugombea maji.
Jumla ya Dola za Kimarekani milioni 350 zimeahidiwa kutolewa na
makampuni mbalimbali ya kimataifa kusaidia taasisi ya Bill Clinton ili iweze
kutekeleza majukumu yake ya kuzisaidia nchi maskini.
Naye mshiriki mmoja wa mjadala wa ajenda hiyo, alisema kuwa wakati
umaefika sasa wa kuzitaka nchi zilizoendelea, Marekani ikiwamo, kubadilika
kifikra na kuwekeza katika usambazaji wa raslimali maji katika maeneo ya
vijijini na mijini.
Alibainisha kwamba
Mwisho