DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
MHESHIMIWA Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa
Aidha, Mheshimiwa Rais, ameagiza kuwa
katika zoezi
Rais Kikwete alitoa maagizo hayo juzi,
Jumanne, Mei 11, 2010 mjini Masasi wakati akipatiwa maelezo ya Maendeleo ya
Mkoa wa Mtwara baada ya kuwa ameambiwa kuwa asilimia 35.6 ya watoto wote 12,843
walioshinda mtihani wa darasa la saba mwaka jana na kuchaguliwa kuingia
sekondari katika mkoa wa Mtwara, hawajaripoti shuleni mpaka sasa.
Rais Kikwete aliambiwa kuwa ni asilimia 64
tu, yaani watoto 8, 278 walioripoti na kuanza masomo ya sekondari wakati watoto
4,565 hawajaripoti shuleni na hawajulikani waliko.
Katika idadi hiyo, Wilaya ya Mtwara ndiyo
inayoongoza kwa asilimia 54, ikifuatiwa na Nanyumbu asilimia 48, Masasi
asilimia 35, Tandahimba asilimia 32, Mikindani asilimia 22 na Newala asilimia
21.
Rais Kikwete aliambiwa na Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara, Kanali (mst) Anatoli Tarimo kuwa baadhi ya sababu zilizowazuia watoto
hao kupiga ripoti shuleni ni pamoja na baadhi
Mara baada ya kupewa takwimu hizo, Rais
Kikwete aliagiza: “Hizi takwimu ni za
juu
Aliendelea kutoa maelekezo Mheshimiwa Rais:
“Tafuteni majina ya watoto hawa wote, wazazi wao waitwe, wajieleze na
“Wazazi wa watoto hao wahojiwe siyo kwa nia
ya kutaka kujua sababu gani zinazuia wasiwapeleke watoto shule, bali kwa nia ya
kuhakikisha kuwa watoto wanapelekwa shuleni mara moja. Kazi hii ifanyike katika
kila wilaya nchini na isimamiwe na mkuu wa wilaya katika kila wilaya ambako
yapo matatizo ya namna hii.”
Rais Kikwete alipewa ripoti hiyo ya
maendeleo ya Mkoa wa Mtwara, ikiwa sehemu ya shughuli zake wakati wa ziara yake
ya siku mbili mkoani humo ambako miongoni mwa mambo mengine jana, Jumatano, Mei
12, 2010, alishirikiana na Rais wa Mozambique, Mheshimiwa Emilio Armando
Guebuza, kufungua rasmi daraja jipya na zuri linalounganisha Tanzania na
Mozambique kwenye Mto Ruvuma.
Daraja hilo lenye urefu wa mita 720, na lililogharimu
kiasi cha shilingi bilioni 34 zilizotolewa kwa usawa na Serikali za Tanzania na
Mozambique, limejengwa kutoka eneo la Mtambaswala kwa upande wa Tanzania kwenda
eneo la Negomane upande wa Mozambique.
Mkataba wa ujenzi wa daraja
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
13
Mei, 2010