UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512,
2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES
SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
leo katika
Ikulu ya Dar-es-Salaam amekutana na kufanya mazungumzo
na Mwakilishi kazi wa Benki
ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) Dr. Tonia Kandiero.
Dr. Kandiero
amefika Ikulu kujitambulisha baada ya kuanza kazi
hapa nchini mwezi Mei, mwaka huu kuchukua nafasi
ya Dr. Sipho Moyo ambaye alimaliza
muda wake hapa Tanzania.
ADB ni moja ya
wahisani wakubwa hapa Tanzania ambapo sehemu kubwa ya
misaada yake inaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo
na hasa sekta
za barabara, Kilimo, Maji na
Nishati.
Dr. Kandiero
pia amefika Ikulu kumueleza rasmi Rais Kikwete
kuhusu mkutano mkuu wa magavana wa benki
hiyo utakaofanyika mjini Arusha tarehe
30 Mei – 01 Juni, 2012.
Mapema kabla ya kuonana
na mwakilishi
wa AFDB, Rais Kikwete amekutana na Balozi Sander Gurbuz wa Uturuki
ambaye amefika Ikulu kumuaga Rais
Kikwete baada ya kufikia ukingoni
mwa muda wake wa kuiwakilisha nchi yake hapa
Tanzania.
Nchi ya Uturuki imefungua
ubalozi wake kwa
mara ya kwanza hapa Tanzania mwaka 2009 na Balozi Gurbuz
ndiye amekua muanzilishi wa Ubalozi huo.
Tangu kufunguliwa kwa
Ubalozi huo, mahusiano baina ya Uturuki na
Tanzania yamekua kwa kiwango kikubwa na miradi mbalimbali
ya maendeleo, kibiashara na kijamii
imeanza na kuimarika katika kipindi chake.
Miradi hiyo ni pamoja na kuanza
kwa safari za ndege kati ya
Tanzania na Uturuki, miradi ya shule
na fursa za mbalimbali za
masomo na biashara baina ya wananchi wa
nchi hizi mbili.
MWISHO.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari
wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
13
Desemba, 2011