TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI WA HESABU KATIKA
AKAUNTI YA MALIPO YA MADENI YA NJE (EXTERNAL PAYMENT ARREARS ACCOUNT – EPA) ILIYOKO BENKI KUU YA
Nafurahi
kuwaarifu kuwa, kazi ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka wa fedha 2005/06 za Akaunti
ya Madeni ya Malipo ya Nje yaani External Payment Arrears (EPA) katika Benki
Kuu ya
Historia ya EPA
Katika miaka ya 1970 mpaka 1990 nchi
yetu ilikuwa inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa fedha za kigeni. Benki Kuu ya
Kwa ajili ya kuwahudumia
wafanyabiashara, mashirika na makampuni yanayoagiza bidhaa na huduma kutoka nje,
Akaunti maalum ilifunguliwa katika Benki ya Taifa ya Biashara kwa wakati huo. Akaunti hiyo ilijulikana kwa jina la External
Payment Arrears (EPA) au Akaunti ya malipo ya Madeni ya Nje, kwa tafsiri ya Kiswahili.
Waagizaji wa bidhaa au huduma kutoka
nje waliwajibika kulipa kwenye Akaunti hiyo, fedha ya
Juni, 1985 iliamuliwa kuwa shughuli
za akaunti hiyo zihamishiwe Benki Kuu
kutoka Benki ya Taifa ya Biashara na zimeendelea kuwepo hapo mpaka sasa. Katika Benki Kuu kikaundwa kitengo maalum cha
kusimamia na kuendesha shughuli za akaunti hiyo kilichojulikana
Kwa sababu ya tatizo la upungufu wa
fedha za kigeni kuendelea, malimbikizo ya madeni hayo yalizidi kukua mwaka hadi
mwaka. Kwa mfano, mwaka 1999 deni
Juhudi za Kulipa Madeni
Juhudi za kulipa malimbikizo ya madeni
hayo ziliendelea kadri fedha za kigeni zilipopatikana. Kwa nia ya kutaka
kutafutia ufumbuzi wa haraka tatizo
Pili, Serikali ilifanya juhudi ya
kupata msamaha wa madeni hayo kutoka nchi wanachama wa Paris Club. Serikali iliomba kuwa pamoja na kutusamehe madeni ya kiserikali toka
nchi zao wasaidie tusamehe na madeni ya makampuni
Ulipaji kwa Idhini
Katika utaratibu wa malipo ya madeni
ya EPA kanuni zinaruhusu mdai kuamua deni
Matatizo
ya Mwaka 2005/6
Katika ukaguzi wa Hesabu za BoT za mwaka wa
fedha 2005/6, Agosti, 2005 kuligundulika matatizo katika ulipaji wa madeni kwa
utaratibu wa idhini ya kulipwa wakala wa mdai katika akaunti ya EPA. Kukajitokeza
kutokuelewana kati ya Benki Kuu na Mkaguzi Deloitte and Touche’ aliyegundua
tatizo
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alifanya hivyo na matokeo ya
mchakato wa kutafuta kampuni hiyo uliochukua miezi mitano (Januari hadi Mei,
2007) ndipo ikapatikana kampuni ya Ernst and Young.
UKAGUZI
Wakaguzi
wa Kampuni ya Ernst and Young wakaanza kazi hiyo Septemba, 2007 na kuikamilisha
Desemba, 2007. Wakaguzi hao wamefanya
kazi nzuri iliyothibitisha kiwango cha juu
cha weledi (Professionalism) cha wakaguzi hao.
Tunawapongeza, tunawashukuru.
Tunatambua kuwa walipata matatizo mengi hasa ya kupata taarifa zilizo
sahihi kwa sababu ya matatizo ya utunzaji wa kumbukumbu. Madeni haya ni ya miaka 27 na zaidi
iliyopita. Kumbukumbu zimehamishwa
kutoka NBC kwenda BoT. Hata huko NBC
shughuli zilikuwa zinafanywa katika matawi mbalimbali nchini tena miaka hiyo hapakuwa
na kompyuta hivyo kumbukumbu zote ziliwekwa kwenye majalada. Pamoja na
matatizo hayo ukaguzi wa hesabu za mwaka
2005/6 ulikamilika kwa kiwango cha kuridhisha.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ukaguzi katika mwaka wa fedha
wa 2005/2006 uliochunguzwa, katika mwaka 2005 yalifanywa malipo ya jumla ya
Shilingi 133,015,186,220.74 kwa Makampuni 22 ya hapa nchini. Makampuni hayo ni: Bencon
International Ltd. of Tanzania, VB & Associates Company Ltd. of Tanzania,
Bina Resorts Ltd. of Tanzania, Venus Hotel Ltd. of Tanzania, Njake Hotel &
Tours Ltd., Maltan Mining Company Ltd. of Tanzania, Money Planners &
Consultants, Bora Hotels & Apartment Ltd., B. V. Holdings Ltd., Ndovu Soaps
Ltd., Navy Cut Tobacco (T) Ltd. of Tanzania, Changanyikeni Residential Complex
Ltd., Kagoda Agriculture Ltd., G&T International Ltd., Excellent Services
Ltd., Mibale Farm, Liquidity Service Ltd., Clayton Marketing Ltd., M/S Rashtas
(T) Ltd., Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloloma and Brothers na KARNEL Ltd.
Aidha, ukaguzi umebaini kwamba kati ya fedha hizo, kiasi cha
Shilingi 90,359,078,804.00 zililipwa kwa makampuni kumi na tatu (13) ambayo
yalitumia kumbukumbu, nyaraka na hati zilizo batili na za kugushi. Hivyo, Makampuni hayo hayakustahili kulipwa
chochote. Makampuni hayo ni: Bencon
International Ltd. of Tanzania, VB & Associates Company Ltd. of Tanzania,
Bina Resorts Ltd. of Tanzania, Venus Hotel Ltd. of Tanzania, Njake Hotel &
Tours Ltd., Maltan Mining Company Ltd. of Tanzania, Money Planners &
Consultants, Bora Hotels & Apartment Ltd., B. V. Holdings Ltd., Ndovu Soaps
Ltd., Navy Cut Tobacco (T) Ltd. of Tanzania, Changanyikeni Residential Complex
Ltd., Kagoda Agriculture Ltd.
Aidha, ukaguzi
umeendelea kubaini kuwa Makampuni tisa (9) ambayo yalilipwa jumla ya Shilingi
42,656,107,417.00 hayakuwa na nyaraka za kuonyesha stahili ya malipo na hivyo
kuwafanya wakaguzi washindwe kuhakiki uhalali wa malipo hayo. Makampuni hayo ni: G&T
International Ltd., Excellent Services Ltd., Mibale Farm, Liquidity Service Ltd.,
Clayton Marketing Ltd., M/S Rashtas (T) Ltd., Malegesi Law Chambers
(Advocates), Kiloloma and Brothers na KARNEL Ltd.
Wakati huo huo
Makampuni mawili, yaani, Rashtas (T) Ltd na G&T International Ltd.,
kumbukumbu zake za usajili katika daftari la Msajili wa Makampuni nchini
hazikuweza kupatikana.
Uamuzi wa Rais
Baada ya
kuipitia Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali na ya Mkaguzi wa Nje,
yaani, Kampuni ya Ernst and Young, Mhe. Rais amesikitishwa na kukasirishwa na
taarifa ya kuwepo vitendo vya ukiukwaji
wa makusudi wa sheria, kanuni na taratibu za uuzaji wa madeni ya nje vilivyofanywa
katika taasisi muhimu na nyeti kama vile Benki Kuu. Kwa hiyo, ameamua kuwa hatua za kisheria na kiutawala zichukuliwe
dhidi ya makampuni na watu waliohusika na vitendo hivyo viovu.
Kwa ajili hiyo
Rais ameamua yafuatayo:-
1. Ametengua uteuzi wa Dkt. Daudi A. Balali kuwa Gavana wa Benki
Kuu ya
2. Ameagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Benki Kuu ikutane mara moja
kujadili taarifa ya ukaguzi na kuchukua hatua zipasazo za kinidhamu dhidi ya
Maofisa wote wa benki, walio chini ya mamlaka yake waliohusika na kusababisha
hasara hii kwa taifa.
3. Shughuli za ulipaji wa madeni katika Akaunti ya EPA
zisimamishwe mara moja mpaka hapo taratibu za uhakiki na utaratibu mpya utakapotengenezwa.
4. Rais amewaagiza; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Inspekta
Jenerali wa Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa, kuchunguza na kuchukua hatua zipasazo za kisheria kwa makampuni na watu
waliohusika na uhalifu huu. Rais
amewataka watumie ipasavyo mamlaka na madaraka waliyo nayo kwa mujibu wa sheria. Aidha, amewataka wakamilishe kazi hiyo katika
kipindi cha miezi sita. Amemuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali awe kiongozi wa
kazi hii. Amewataka wahakikishe kuwa fedha
zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.
5. Rais pia amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali kushirikiana na kuwasaidia watendaji wakuu hao wa vyombo vya dola
katika kufanikisha jukumu lao
6. Kutokana na hatua ya
kutengua uteuzi wa Bwana BALALI, Mhe. Rais amemteua Prof. BENNO T. NDULU (Naibu
Gavana) kuwa Gavana Mpya wa Benki Kuu.
Halikadhalika, amemteua Dkt. ENOS S. BUKUKU (Katibu Mkuu – Miundombinu)
kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu (Fedha na Uchumi). Pia amemteua Ndugu Omari Chambo kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Miundombinu. Uteuzi huu unaanza mara moja.
(Phillemon L. Luhanjo)
KATIBU
MKUU KIONGOZI
IKULU,
DAR ES
SALAAM
09 Januari 2008