DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail : press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
Ben Mtobwa alikuwa mwanataaluma
mzalendo – Rais Kikwete
RAIS Jakaya Mrisho
Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwandishi wa habari na
vitabu maarufu nchini, Ben Mtobwa, aliyefariki dunia Jumapili iliyopita,
Novemba 9 2008, mjini Dar Es Salaam.
Rais amemwelezea
marehemu kama mwanataaluma mzalendo ambaye aliitumia kalamu yake kwa busara na
kwa ajili ya kuleta maelewano ndani ya jamii ya Tanzania.
Katika salamu hizo,
Rais Kikwete ameieleza familia hiyo: “Naungana nanyi wote katika wakati huu mgumu na wa majonzi makubwa
mliyonayo kwa msiba huo mkubwa uliowapata. Tunaelewa machungu mliyonayo”
Amesisitiza Rais
Kikwete katika salamu hizo za rambirambi: “Nimemjua marehemu Mtobwa kwa miaka mingi
katika ujenzi wa taifa letu, hususan katika masuala yaliyohusu utaalamu wake wa
masuala ya habari na uandishi.”
“Marehemu Mtobwa
alikuwa wanataaluma mzalendo, aliyetumia kalamu yake kwa busara na kwa nia ya
kuleta maelewano ndani ya jamii yetu. Alijali maadili ya taaluma yake na
kutimiza vyema wajibu wake katika jamii kwa mujibu wa maadili hayo.”
Amemalizia Rais
Kikwete: “Naungana nanyi wote katika kuomboleza msiba huu mkubwa. Kwa pamoja
tumshukuru Mungu kwa kumwezesha Ndugu Mtobwa kutoa mchango wake kwa taifa
letu.”
Marehemu Mtobwa
anatarajiwa kuzikwa leo kwenye shamba lake Bunju A mjini Dar Es Salaam.
Mwisho
Imetolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano
Ikulu.
Dar es Salaam.
12 Novemba, 2008