
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY TO THE
PRESIDENT
Fax. No. 255-22 2113425 The State House,
Tel: 255-22-2116539/2116913 P.O. Box 9120,
DAR ES
SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz
Premi
Kibanga,
Copenhagen,
Denmark
2 March, 07
Mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini Tanzania ni
kipimo bora na mfano wa kuigwa na nchi
zote barani Afrika.
Waziri Mkuu wa Denmark Bwana. Anders Fogh
Rasmusssen amemweleza Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana (1.March .07) wakati wa
mazungumzo mjini hapa.
“Umefanya mabadiliko makubwa na tumevutiwa sana na matokeo yaliyopatikana hadi sasa, tunatiwa moyo sana na serikali yako,
imeweka kiwango cha mafaniko ambacho kinafaa kuigwa na nchi zote barani
Afrika”. Amesema na kuongeza kuwa “ Kutokana na jitihada hizo za Tanzania,
tumeamua kutayarisha sera mpya ya Afrika yenye lengo la kukuza mahusiano yetu
kwa miaka ijayo”.
Bwana Rasmussen amesema Denmark imeazimia kuongeza misaada
kwa nchi za Kiafrika ili kujenga mahusiano imara yenye lengo la kuendeleza
mabadiliko haya ya kisiasa na kiuchumi,
ili kujenga mazingira bora katika
masoko, biashara na pia katika kukuza
amani na utulivu barani Afrika.
Rais Kikwete amemweleza kwa undani jitihada za serikali
yake katika kuendeleza na kuimarisha marekebisho ya kisiasa ambapo ameelezea
hatua zilizofikiwa katika maswala ya utawala bora haswa suala la kupambana na
rushwa, swala ambalo Denmark imesema
imeridhishwa sana nalo na kwamba ni swala lililowazi kuwa serikali ya Tanzania imedhamiria na hivyo kuifanya Denmark nayo
kurejea ahadi zake za kuendelea kuisaidia Tanzania bila mjadala zaidi.
“Mahitaji yote yakikamilika na kuwa wazi Denmark itatoa msaada wake kama ilivyokwisha
kubalika” Amesema Bw. Rasmussen na kuongeza kuwa mbali na kuongeza misaada kwa Tanzania, Denmark itatoa kipaumbele kwa elimu
kwa watoto wa kike ili kuimarisha nafasi za wanawake katika maendeleo.
Mwishoni mwa mwaka jana Denmark
ilizuia mchango wake wa asilimia ishirini kwa Tanzania
kwa kile kilichodaiwa kuchelewa kuwakilisha bungeni mswaada wa marekebisho ya
sheria ya kupambaba na rushwa Tanzania,
muswaada ambao tayari umeshawakilishwa mwezi Februari mwaka huu na unatarajiwa
kuwa ufikapo mwezi wa Mei utakuwa umekamilika.
“Tutaendeleza marekebisho haya na pia tumedhamiria kujenga uchumi imara na tulivu
lakini tuna changamoto kubwa ya kuikomboa sekta binafsi na kuijengea mazingira
mazuri kama vile kupata mikopo na mitaji.”
Amesema Tanzania
imeingia katika awamu ya pili ya marekebisho ya sekta ya fedha yenye lengo la
kuwezesha wananchi na sekta binafsi kupata mitaji na mikopo kwa lengo la
kuendeleza sekta za kilimo, utalii, madini,
nishati na sekta mbalimbali za kutoa huduma.
Viongozi pia wamezungumzia maswala mbalimbali ya Afrika
ikiwemo swala la Dafur, Zimbabwe na juhudi mbalimbali za Tanzania katika
kuleta amani na utulivu barani.
“Tanzania
imekuwa mstari wa mbele barani katika kuleta amani na utulivu, mambo ambayo ni
muhimi kwa maendeleo. Tunaunga mkono na tutazidi kusaidia Afrika katika swala
hili” Amesema.
Rais anatarajia kukamilisha ziara yake hapa Denmark leo kwa kukutana na mume wa Malkia
Margrette II wa Denmark,
Prince Henrik na viongozi wengine wa juu serikalini akiwemo Waziri wa
Ushirikiano wa Maendeleo Mama Ulla Tornaes.Rais anatarajiwa kurejea nyumbani
kesho (3.02. 07)
Ends