UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Zanzibar Mheshimiwa Dr. Ali Mohammed Shein,
ameapishwa na Jaji Mkuu wa
Tanzania kwa ajili ya kushiriki vikao
vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Hii
ni kutokana
na Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kifungu 54 ibara ya kwanza ambayo inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri
kuwa ni Makamu
wa Rais, Waziri Mkuu, Rais
wa Zanzibar na Mawaziri wote.
Kiapo
hicho kimeshuhudiwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu, Mwanasheria
Mkuu, Mawaziri na maafisa wengine
serikalini.
Mara baada ya kula
kiapo hicho, Rais Wa
Zanzibar amehudhuria kikao
cha Baraza la Mawaziri kikiongozwa na Rais Kikwete.
Mara baada ya Baraza
la Mawaziri kukamilika jioni leo,
Rais anatarajiwa kuelekea Perth, Australia kuhudhuria
Kikao cha Nchi Wanachama wa Jumuiya
ya Madola kinachofanyika kuanzia tarehe 28-30 mwezi huu.
Kabla
ya Mkutano Mkuu kuanza, tarehe
25 Oktoba, kutakuwa na vikao kadhaa kikiwemo kikao cha wafanyabiashara ambacho Rais Kikwete
anatarajiwa kutoa hotuba ya ufunguzi na baadaye kujumuika na viongozi kadhaa
wa nchi chache katika kikao
maalum na wafanyabiashara.
Rais
anatarajiwa kurejea nchini tarehe 3 Novemba, 2011.
Mapema
leo asubuhi Rais amepokea Hati
za Utambulisho kutoka kwa mabalozi
wa n chi za Sudan na Japan.
Balozi
Mteule wa Sudan Bw. Yassir Mohamed Ali amewakilisha hati zake kwanza na kufuatiwa na Balozi
Masaki Okada.
Mwisho.
Imetolewa
na Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari
wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
24
Oktoba, 2011