DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512,
2116898 E-mail : press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Tumeona
ni vizuri kuwashirikisha katika tukio hili la kuwakabidhi viongozi wa chama cha
Maalbino
Mtakumbuka
tarehe 19 Oktoba, 2008 wakati Rais alipopokea maandamano ya kulaani mauaji ya
maalbino, pamoja na mambo mengine aliahidi kutoa jezi na vifaa vingine vya
michezo kwa timu ya maalbino itakayocheza mechi ya kirafiki na waheshimiwa
wabunge leo tarehe 26 Oktoba, 2008 katika uwanja wa taifa.
Vyombo
vya habari vimekuwa ni wadau na washiriki wakubwa katika kufichua vitendo vya
ukatili na unyayapaa wanavyofanyiwa maalbino.
Mheshimiwa Rais anazidi kuwapongeza kwa juhudi zenu katika kipigania
haki za maalbino.
Rai
yetu ni kwamba tunaomba kwa pamoja tuendeleze ujumbe kwamba maalbino ni
binadamu
Hii
ndiyo maana Mheshimiwa Rais ameamua kutoa jezi 33 na vifaa vinavyohusiana na michezo
vyenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili Laki Moja Arobaini na Tatu Elfu (Shs.
2,143,00/=) kwa maalibino ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu mechi ya leo
kati yao na waheshimiwa wabunge.
Ahsanteni
Kisare
Makori,
Kaimu
Mkurugenzi,
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26
Oktoba, 2008