UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116539

E-mail: press@ikulu.go.tz

Website:  www.mawasilianoikulu.go.tz  

Fax: 255-22-2113425

 

Coat of Arms

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Machi 25, 2011, ametia saini kitabu cha maombolezo kufuatia upotevu wa maisha ya maelfu kwa maelfu ya wananchi wa Japan ambao wamepoteza maisha yao katika tsunami na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Machi 11, mwaka huu, nchini humo.

 

Rais Kikwete ametia saini kitabu hicho jioni ya leo kwenye Ubalozi wa Japan ulioko Upanga, mjini Dar es Salaam.  Pamoja naye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe ambaye naye ametia saini kitabu hicho.

 

Kwenye ubalozi huo, Rais Kikwete amepokelewa na Balozi wa Japan katika Tanzania Mheshimiwa Hiroshi Nakagawa na maofisa wengine wa ubalozi huo.

 

Akizungumza kwa ufupi tu baada ya kuwa ametia saini kitabu hicho, Rais Kikwete ametoa salamu za rambirambi kwa nchi hiyo ya Japan ambayo ameielezea kama rafiki wa siku nyingi kwa upotevu mkubwa wa maisha na mali kutokana na tsunami iliyoambatana na tetemeko kubwa la ardhi.

 

Mara tu baada ya tukio hilo la huzuni kubwa, Serikali ya Tanzania ilituma salamu rasmi za rambirambi kwa Serikali ya Japan.

 

Mwisho.

 

Imetolewa na:

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

 

25 Machi, 2011