DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS Jakaya Mrisho
Kikwete amefanya mabadiliko katika safu ya maofisa waandamizi wa Serikali kwa
kuteua Makatibu Wakuu wa Wizara wanne wapya, kuhamisha wengine wawili, na
kuteua Katibu wa Rais mpya.
Taarifa iliyotolewa
leo, Jumatatu, Oktoba 19, 2009, Ikulu, mjini
Aidha, taarifa
inasema kuwa mabadiliko hayo yanaanza leo, Oktoba 19, 2009.
Taarifa hiyo
imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana David Kitundu Jairo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Jairo alikuwa Katibu wa Rais.
Bwana Jairo
anachukua nafasi ya Bwana Arthur
Mwakapungi ambaye amestaafu.
Katika taarifa
yake, Bwana Luhanjo amesema kuwa pia Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Sazi Salula kuwa Katibu Mkuu wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Salula alikuwa
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Taarifa hiyo pia
imesema kuwa Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Mbarak M. Abdulwakil aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu
wa Rais, kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Bwana Abdulwakil
anachukua nafasi ya Bwana Patrick
Rutabanzibwa ambaye anahamishiwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi
Kwa mujibu wa
taarifa hiyo, Mhe. Rais Kikwete pia amemteua Bwana Christopher N. Sayi kuwa Katibu Mkuu wa Wizata ya Maji na
Umwagiliaji.
Kabla ya uteuzi
wake, Bwana Sayi alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo hiyo, na
anachukua nafasi ya Bwana Wilson Mukama ambaye ameanza likizo ya kustaafu kwa
mujibu wa sheria.
Bwana Luhanjo
amesema katika taarifa yake kuwa vile vile Mhe. Rais Kikwete amemteua Bwana Sethi Kamuhanda kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.
Kabla ya uteuzi
wake, Bwana Kamuhanda alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.
Anachukua nafasi
Dkt. Florence Turuka ambaye anahamishiwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia
Taarifa ya Katibu
Mkuu Kiongozi pia inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prosper Mbena kuwa Katibu wa Rais. Kabla ya uteuzi wake, Bwana
Mbena alikuwa Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, na anachukua nafasi ya
Bwana Jairo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
19 Oktoba, 2009