DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Na Mwandishi Maalum
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Machi 12, 2009, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk Donald Kaberuka kuhusu masuala mbali yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Benki hiyo.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Rais Kikwete amemwambia Rais huyo wa AfDB kuwa Tanzania inafurahishwa na kuridhishwa na uhusiano uliopo kati yake na Benki hiyo.
Rais pia amemshukuru Kaberuka kwa misaada ambayo Benki hiyo imekuwa inatoa katika eneo la ufundishaji wa masomo ya sayansi nchini, na kuongeza kuwa Tanzania itahitaji kuzidi kusaidia zaidi katika eneo hilo.
Rais Kikwete pia ameishukuru pia Benki hiyo kuwa msaada wake wa fedha katika eneo la miundombinu, na katika maandalizi ya kujengwa kwa reli mpya kati ya Isaka na Kigali, Rwanda.
“Reli hii ni mradi mwingine mkubwa kwetu. Ni suala la kufa ama kupona. Ni reli muhimu sana na kunathamini sana msaada wetu katika eneo hili kwa sababu tunahihitaji reli hii,” Rais Kikwete amemwambia kiongozi huyo wa AfDB.
Viongozi hao pia wamezungumzia hali ya utendaji wa sekta ya fedha katika Tanzania katika hali ya sasa ya matatizo makubwa ya kiuchumi na kifedha duniani na kuridhika kuwa bado mabenki ya Tanzania yako katika hali nzuri.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
12 Machi, 2009