UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.com

              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

Coat of Arms

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

              P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 5, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na Masheikh wa Dini ya Kiislam kuhusu mchakato wa kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini.

 

Katika mkutano huo, pande hizo mbili zimezungumzia kwa undani hali ya majadiliano ya suala zima la kuanzishwa kwa Mahakama hiyo ya Kadhi.

 

Mheshimiwa Rais na Masheikh wamekubaliana kuwa Kamati ya Pamoja ya Serikali na Masheikh ikutane mapema iwezekanavyo na iongeze kasi ya majadiliano ili shughuli hiyo iweze kumalizika mapema iwezekanavyo.

 

(Habari hii imeambatana na picha ya Mheshimiwa Rais na Masheikh katika kikao hicho cha jana).

 

Imetolewa na:

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

 

06 Septemba, 2011