UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
TANZANIA na Uganda zimekubaliana kuharakisha ujenzi wa reli ya
Tanga-Musoma-Uganda ili kuhitimisha ndoto ya miaka
mingi ya Mwanzilishi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Nchi hizo mbili pia
zimekubaliana kupanua bandari za Tanga
na Musoma
katika Tanzania, na kujenga bandari mpya nchini Uganda ili kuhudumia reli
hiyo mpya kati ya nchi
hizo mbili.
Hayo ndiyo yalikuwa maamuzi makuu yaliyofikiwa
leo, Jumatatu, Oktoba 3, 2011, katika mkutano kati ya
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
na Rais wa
Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Museveni ambaye amefanya ziara ya kikazi ya
siku moja nchini Tanzania amewasili leo asubuhi
na kupokea na mwenyeji wake Rais Kikwete kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kiongozi huyo wa Uganda ameondoka kurejea nyumbani baada ya mazungumzo
na mwenyeji wake.
Wakati wa mazungumzo
yao, viongozi hao wawili wamekubaliana
kuharakisha ujenzi wa reli hiyo
kama njia ya kufungua mlango
wa tatu wa
Uganda kupitishia bidhaa zake kutoka na
kwenda kwenye Bahari ya Hindi. Milango mingine inayotumiwa na
Uganda kusafirisha bidhaa kutoka na kwenda
Bahari ya Hindi ni bandari za
Dar es Salaam na Mombasa,
Kenya.
Katika kuhakikisha uamuzi wake wa kuharakisha
ujenzi huo unaanza katika muda mfupi iwezekanavyo,
viongozi hao wawili wameunda kikosikazi cha kusimamisha suala hilo. Kikosi
kazi hicho kitaundwa na
mawaziri wa wizara za usafirishaji
na uchukuzi, fedha na mambo ya nje kwa
kila nchi.
Chini ya mpango huo,
bidhaa zitasafirishwa kwa reli
kutoka Bandari ya Tanga hadi
Bandari ya Musoma na kuwekwa
kwenye pantoni maalum ya (wagon ferry) reli kutoka Bandari
ya Musoma hadi bandari mpya
ya Uganda kwa kuvushwa Ziwa Victoria.
Viongozi hao wamefanya uamuzi
wa kuharakisha
ujenzi huo kwa sababu ya
faida za reli hiyo kwa
chumi za nchi zote mbili
lakini pia kwa kujua kuwa
bila usimamizi wa karibu wa
Tanzania na Uganda itachukua
miaka mingi zaidi kwa reli
hiyo kuweza kujengwa.
Wazo la kujenga reli ya
kuunganisha Uganda na Bandari ya Tanga kupitia
Bandari ya Musoma liliasisiwa miaka mingi tokea
awamu ya kwanza ya uongozi wa
Tanzania, lakini kwa namna moja ama
nyingine, utekelezaji wa wazo hilo
umekumbana na changamoto mbalimbali.
Katika mkutano wao wa leo, viongozi
hao pia wamejadili
masuala mengine yanayohusu uhusiano kati ya nchi
hizo mbili na masuala mengine
ya kikanda na kimataifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
03
Oktoba, 2011