UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mfumo
wa Mawasiliano
ya Kompyuta kwa Kiswahili wazinduliwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
usiku wa jana, Jumanne, Mei 24, 2011 alizindua rasmi Mfumo wa Mawasiliano
ya Komptyuta wa Windows 7 Kiswahili Interface Pack unaotumia
lugha ya Kiswahili na unaotarajiwa kunufaisha zaidi ya watu 150 milioni wanaozungumza Kiswahili kote duniani.
Sherehe za uzinduzi wa Mfumo
huo wa Mawasiliano
zilifanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa
miongoni mwa wageni wengine Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Meneja Mkuu wa Microsoft Kanda ya Afrika Mashariki
na Kati.
Katika uzinduzi
huo, Rais Kikwete amesema Mfumo huo wa
Mawasiliano kwa njia ya Kompyuta
unaotumia Lugha ya Kiswahili, umefungua ukurasa mpya wa
historia ya maendeleo ya teknolojia
ya habari na mawasiliano na ya matumizi
ya Lugha ya Kiswahili, kwani kwa mara ya
kwanza lugha hiyo inapewa nafasi sawa na lugha
nyingine kubwa duniani zinazotumika kwa kupashana habari
na mawasiliano kwa njia ya
kompyuta.
Rais Kikwete
ameipongeza na
kuishukuru Kampuni ya Microsoft kwa kutambua na kuthamini
umuhimu wa Lugha ya Kiswahili. “Uamuzi wenu huo utasaidia
sana katika kukuza na
kuendeleza Lugha ya Kiswahili”, amesema Rais Kikwete na
kuongeza, “utawafanya wale ndugu zetu wanaobeza
na kutotaka kuendeleza matumizi ya Lugha ya
Kiswahili katika elimu, sayansi, teknolojia na shughuli za
serikali na biashara kuwa na
mawazo tofauti.
Amesema upatikanaji
wa programu
ya kompyuta ya Windows 7, utawawezesha watumiaji wa Kiswahili duniani kunufaika na matumizi ya
lugha wanayoielewa zaidi katika kompyuta
na hivyo kuondokana na kikwazo
cha lugha, kwani watajipatia elimu na maarifa kupitia
mitandao ya kompyuta na pia
kurahisisha mawasiliano kwa njia ya
baruapepe.
Mfumo wa Mawasiliano kwa njia ya
Kompyuta unaotumia Lugha ya Kiswahili kwa kiasi kikubwa
umetengenezwa na Watanzania wenyewe ambao wametafsiri zaidi ya maneno
300,000 ya kiufundi yaliyomo kwenye Microsoft Windows
7 Glossary kwenda kwenye Lugha ya Kiswahili wakishirikiana na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na
Kampuni yenyewe ya Microsoft. Programu hii ya Kompyuta
inategemewa kusambazwa kwenye taasisi zote za elimu
hapa nchini.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25
Mei, 2011