DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mhe. Rais Jakaya
Kikwete amemteua Jaji Frederick Mwita Werema kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Aidha, Mhe. Rais
Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
Uteuzi huo unaanza
leo, Jumanne, Oktoba 20, 2009.
Kabla ya uteuzi
wake, Jaji Werema alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya
Jaji Werema
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Johnson Mwanyika ambaye yuko kwenye
likizo ya kustaafu kwa mujibu wa sheria. Bwana Mwanyika aliteuliwa kuwa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Desemba, mwaka 2005.
Naye Bwana Masaju
kabla ya uteuzi wake alikuwa Mshauri wa Sheria wa Rais, Ikulu.
Wakati huo huo,
Mhe. Rais Kikwete kesho, Jumatano, Oktoba 21, 2009 atawaapisha maofisa hao
wawili waandamizi wa Serikali pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara za Serikali
ambao aliwateua jana, Jumatatu, Oktoba 19, 2009.
Maofisa hao watakaoapishwa
ni Jaji Frederick M. Werema kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Bwana David
Kitundu Jairo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Bwana Sazi Salula
kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa; na Bwana
Mbarak M. Abdulwakil kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wengine
watakaoapishwa ni Bwana Christopher Sayi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na
Umwagiliaji; Bwana Sethi Kamuhanda kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Habari,
Utamaduni na Michezo; Bwana Prosper Mbena kuwa Katibu wa Rais, na Bwana George
Masaju kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Shughuli ya
kuapishwa itaanza saa sita mchana, Ikulu,
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
20 Oktoba, 2009