DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mhe. Rais Jakaya
Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Oktoba 5, 2009, ametoa mwito maalum kwa
Watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha, ili waweze kushiriki kuwapigia
kura viongozi wa serikali za mitaa.
Mhe. Rais Kikwete
ametoa mwito huo wakati yeye mwenyewe alipojiandikisha katika Kituo cha Shule
ya Msingi ya Bunge karibu na Ikulu, Dar e Salaam, ili aweze kupiga kura katika
uchaguzi huo uliopangwa kufanyika nchini kote baadaye mwezi huu, Oktoba 25,
2009.
Aidha, Mhe. Rais
ametaka wananchi kuwakemea baadhi ya watu wachache ambao wamekuwa wanafanya
fujo katika zoezi la uteuzi wa wagombea katika uchaguzi huo na kwenye zoezi la
uandikishaji.
mesema Mhe. Rais baada ya kuwa amejiandikisha:
“Niwaombeni Watanzania kote nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha. Hatari
ni kwamba watu wanaweza kupuuza uchaguzi huo wakingojea ule wa Rais na wabunge
mwakani.”
Amesisistiza:
“Lakini kila uchaguzi una uzito wake na viongozi hawa tutakaowachagua baadaye
mwezi huu ndiyo viongozi muhimu katika maisha yetu. Hawa ndio tunaishi nao kila
siku.
“Hivyo, nawaombeni
Watanzania tujitokeze kwa wingi kujiandikisha na siku ile ya Oktoba 25,
tujitokeze kwa wingi kupiga kura. Watu wasije kupuuza zoezi
“Hawa ndio viongozi
wa shida zetu za mchana na usiku. Nawaombeni
Mhe. Rais amesisitiza kuwa katika kuboresha
mfumo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, zamu hii Serikali imeanzisha daftari la
wapigaji kura badala ya huko nyuma ambako watu walikuwa wanapiga kura bila
kujiandikisha kwenye daftari.
“Uchaguzi uliopita
hakukuwapo na daftari la wapigaji kura. Lakini ili kuondoa malalamiko ya aina
yoyote, zamu hii tumeanzisha daftari
Alipoulizwa na
mwandishi wa habari juu ya fujo ambazo zimekuwa zinaripotiwa na vyombo vya
habari kuhusiana na uchaguzi huo, Mhe. Rais amesema:
“Binafsi nawashangaa watu wanaofanya fujo. Shughuli yenyewe haitakiwi kuwa na fujo. Ni
jambo lisilokuwa na maana na kwa kweli ni ukosefu wa busara watu kufanya fujo
katika zoezi hili. Tukemee jambo hili. Tuwakemee watu hawa wanaofanya fujo za
kijinga. Ni lazima waache uhuni.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
05 Oktoba, 2009