DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mheshimiwa RAIS Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumapili, Oktoba 4, 2009, amelazimika kupumzika kwa dakika
chache katika chumba cha mapumziko kwenye Uwanja wa
Kirumba, mjini Mwanza, mara tu
baada ya kumaliza hotuba yake wakati wa
sherehe za miaka 100 tokea kuanzishwa kwa Kanisa la African Inland
Church (AIC) katika Tanzania.
Mhe. Rais amelazimika kupumzika kutokana na kuzidiwa
na uchovu kufuatia shughuli nyingi mfululizo katika siku za
karibuni. Baada ya mapumziko hayo, Mhe. Rais aliendelea kushiriki katika shughuli hizo hadi
mwisho wa
shughuli hiyo ya AICT.
“Nguvu imerudi…napenda
sasa kuchukua nafasi hii kuzindua
rasmi uchangiaji wa shughuli za
Kanisa lenu na mimi naanza
na mchango wa sh. 1,000,000,” Rais Kikwete amewaambia maelfu ya waumini
wa AICT huku wakimshangilia kwa nguvu mara aliporejea
jukwaani.
Rais Kikwete amekuwa na shughuli
nyingi na hajapumzika katika miezi kadhaa iliyopita
kutokana na kazi nyingi na
ratiba ya shughuli za mfululizo.
Aidha ndani ya siku 15 zilizopita,
Rais Kikwete amekuwa New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York, na juzi na jana
alikuwa mjini Arusha na jana
na leo mjini
Mwanza.
Rais ameanza kusikia uchovu wakati akisoma
hotuba yake mbele ya maelfu
ya waumini wa Kanisa
Baada ya kuwa amemaliza
hotuba hiyo ameingia katika chumba cha kupumzika kwa dakika
chache na baadaye akarudi kujiunga na waumini
hao kuendelea na sherehe hizo.
Rais Kikwete ameendelea kubakia kwenye sherehe hizo hadi
mwisho wa
ratiba yake na wakati akiwaaga
waumini hao amesema:
“Kwa kweli mshituko
huu wa
leo ni matokeo
ya ubishi wangu. Nilishauriwa na wasaidizi
wangu nipumzike baada ya kurejea
nyumbani kutoka Marekani. Niliambiwa nisiende Arusha
ama kuja hapa. Lakini nikakataa. Siku nyingine
nitawasiliza zaidi.”
Rais Kikwete aliondoka kwenda Marekani kuhudhuria Mkutano wa Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) Septemba 20 na tokea hapo hajapata
kupumzika.
Alirejea nchini kutoka Marekani
saa saba
usiku wa kuamkia Ijumaa baada ya kuwa
amesafiri kwa zaidi ya masaa
19 na asubuhi ya Ijumaa akasafiri
kwenda Arusha kufungua Mkutano wa 55 wa Wabunge
wa Jumuia ya Madola.
Rais alikuwa amepangiwa kurejea Dar es Salaam baada ya shughuli
ya Arusha, lakini akalazimika kwenda Mwanza kwa shughuli ya Kanisa la AICT kwa sababu Waziri
Mkuu aliyekuwa amepangiwa na Rais
kushiriki shughuli hiyo alipewa kazi
nyingine na Rais.
Wakati
huo huo, Ofisi Binafsi ya
Rais (OBR) imetangaza kuwa itaangalia upya ratiba ya
Mhe. Rais kwa namna
ya kumpungumzia mlundiko wa shughuli
hata
Ofisi
hiyo ndiyo husimamia kupanga ratiba za Mhe. Rais na baada ya tukio
la leo imetangaza kuwa inaangalia upya ratiba nzima
ya matukio yajayo ya Mhe.
Rais kwa
namna ya kuyapunguza na kumpa muda zaidi
wa kupumzika.
Hata hivyo, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba Mhe. Rais ni mzima wa afya
na anaendelea vizuri.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Oktoba, 2009