DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, jana, Jumatano, Juni 9, 2010, alikutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya (EU), Mheshimiwa Karel De Gutch.

 

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete na Mheshimiwa De Gutch walijadiliana kuhusu masuala mbalimbali na hasa kuhusu hali ya majadiliano ya jinsi ya kufikia mkataba mpya wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na EU.

 

Pande hizo mbili zimekuwa zinajadiliana kuhusu vipengele mbalimbali vinavyokubaliwa na pande hizo mbili ili viwekwe katika Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi (EPA) kati ya pande hizo mbili.

 

Wakati huo huo, Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na mtaalam wa shughuli za uchumi kutoka Marekani, Dkt. Sarah Moten.

 

Mama huyo ni mmoja na watu ambao waliisaidia sana Tanzania katika nyanja ya elimu wakati alipokuwa mwajiriwa wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani la USAID.

 

Imetolewa na:

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

 

10 Juni, 2010