UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama Cha National
Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR-Mageuzi)
kimempongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete
kwa kusimamia
suala la Katiba vizuri na kwa
umakini mkubwa.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bwana James Mbatia ametoa pongezi hizo leo jioni
alipofika Ikulu, akiongoza ujumbe wa viongozi wenzake
sita(6),
kuja kujadili suala la Katiba Mpya ya Tanzania.
"Tunakupongeza kwa kusimammia suala la Katiba vizuri, ni suala
zito ambalo litatupa uhai vizazi
na vizazi vijavyo". Amesema kama utangulizi
wa ujio wao
Ikulu.
"Upinzani sio uadui, tunahitaji kufanya marekebisho ya Katiba kwa amani na hoja bila
kuvuruga amani yetu” Bwana Mbatia amesema na kuongeza
kuwa “suala la Katiba linahitaji ushirikiano wa pamoja kwa nia
njema, kwani taifa hili ni
letu sote" ameeleza.
Akiwakilisha
hoja ya NCCR-Mageuzi kwa
Rais Kikwete, Mkuu wa Idara
ya Sheria wa NCCR-Mageuzi Dkt. Senkondo Mvungi
amesema, NCCR - Mageuzi inatambua ukubwa wa jambo hili
la wa Tanzania kupata Katiba.
"Ni jambo kubwa sana, wewe
ndiyo Rais wa kwanza kutengeneza sheria ya kupata
katiba mpya na kuanzisha Mchakato
wa kupata Katiba Mpya.
Kikao
cha leo cha Rais na viongozi
wa NCCR-Mageuzi ni mwendelezo wa
jitihada za Rais Kikwete, kusikiliza,
kuchukua maoni na mawazo ya
wadau mbalimbali kutoka vyama vya
siasa, asasi za kijamii na
makundi mbalimbali katika kuelekea mchakato wa kupata
Katiba Mpya ya Tanzania.
Rais amesema kuwa nchi hii
inayo Katiba ambayo imelilea vizuri na kulifikisha
Taifa la Tanzania hapa lilipo, lakini pia Taifa linahitaji
Katiba inayoendana na wakati na
itakayoweza kulilea Taifa hili kwa
miaka mingi ijayo.
Mara baada ya kumaliza
kikao na viongozi wa NCCR-Mageuzi, Rais Kikwete
amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
ikiwa ni mwendelezo wa mazungumzo
yao yalioanza mwishoni mwa mwezi
Novemba mwaka 2011, kuhusu Katiba Mpya
ya Tanzania.
Katika mazungumzo haya na Vyama vya Siasa
Rais amesisitiza kuwa lengo la mazungumzo
haya yote ni kuhakikisha kuwa hatimaye Watanzania
wote watakiri kuwa Katiba Mpya
ni yao wote
na hatimaye ifikapo mwaka 2015 nchi iweze kufanya
uchaguzi wake na Katiba Mpya.
Mwisho.
Imetolewa na
Premi Kibanga,
Mwandishi
wa Habari
Msaidizi wa Rais,
Ikulu.
Dar
es salaam.
21 Januari, 2012