UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano
wa Viongozi Wakuu wa Vyama
vya Siasa vilivoshiriki katika Ukombozi Kusini mwa Afrika, umekubaliana
kuweka kumbukumbu na kuhifadhi yaliyokuwa maeneo yao makuu
yaliyotumika wakati wa harakati za
ukombozi.
Vyama
hivyo vimekutana mjini Windhoek, Namibia tarehe 11 Agosti, 2011 chini ya uenyekiti wa Rais wa Namibia,
Dr. Hifikepunye Pohamba ambaye pia ni Rais wa Chama kinachotawala cha SWAPO.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama
Cha Mapinduzi ameshiriki na kuelezea kuunga mkono uamuzi
huo wa kuainisha
maeneo hayo muhimu ambayo mengi
yako nchini Tanzania kutokana na mchango wake mkubwa
katika ukombozi wa bara la Afrika.
« Tumekubaliana kila Chama kiainishe na kuyatambua maeneo yake muhimu
kwa ajili ya kulihifadhi kama kumbukumbu na historia ya nchi hizi, ambapo
Tanzania tutasaidia katika kuyatambua lakini suala la kuyagharamia itakua jukumu la nchi husika ». Rais amesema.
Nchini
Tanzania maeneo ya historia
ya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika
yako katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu ikiwemo
Chunya, Kongwa, Morogoro na
Nachingwea.
Vyama
vingine vilivyoshiriki katika mkutano huo wa viongozi
ni Chama cha ZANU-PF kikiongozwa na Katibu wake Mkuu
wa Kwanza ambaye pia ni Rais wa Zimbabwe, Rais
Robert Mugabe, Chama cha
MPLA, kimewakilishwa na Makamu wa Rais wa chama
hicho Ndugu Robert De
Almeida akimwakilisha Rais wa
MPLA ambaye pia ni Rais wa Angola Rais Jose Eduardo Dos Santos.
Chama
cha ANC kikiwakilishwa na Katibu Mkuu wake
Ndugu Gwede Mantashe, ambaye amemwakilisha Rais wa ANC ambaye pia ni Rais wa Afrika ya Kusini,
Rais Jacob Zuma na FRELIMO chini
ya Katibu wake Mkuu Ndugu Filipe Paunde akimwakilisha Rais wa FRELIMO ambaye pia ni Rais wa Msumbiji Rais Armando Guebuza.
Pamoja
na mambo mengine vyama hivi vimekutana kwa nia ya kuimarisha mahusiano baina ya vyama hivi ambavyo
vina historia kubwa na muhimu
sana katika Nchi za Kusini mwa
Afrika.
Rais Kikwete na ujumbe wake wamerejea Dar-Es-salaam jana jioni (11 Agosti, 2011) mara baada ya kikao
hicho cha siku moja kukamilika
MWISHO
Imetolewa
na Premi Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais Msaidizi
Windhoek, Namibia
11
Agosti, 2011