DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mwaka
2011 umeelezewa kuwa Mwanzo wa
Muongo wa Vita Dhidi ya Malaria Barani Afrika. Rais Jakaya Mrisho
Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mshikamano
wa Viongozi wa Afrika Dhidi
ya Malaria (African Leaders Malaria Alliance-ALMA),
amesema leo mchana wakati akifungua
Kikao cha Viongozi wa Nchi 35 za
Afrika zinazounda Mshikamano wa Kupambana
na Malaria Barani Afrika. “Mwaka wa
2011 ni Mwanzo wa Muongo Mpya
katika Afrika Dhidi ya Malaria, pia unaashiria mstari wa mwisho
katika kukaribia mwisho wa juhudi
hizi katika kufuta vifo vinavyotokana
na malaria kuelekea mwaka 2015”.
Rais
Kikwete amesema na kuelezea
umuhimu wa hatua hii iliyopigwa
na nchi za
Afrika katika kufikia malengo ya milenia ambayo
yamewekwa na nchi hizi kama
wanachama wa familia ya Umoja
wa Mataifa. Kulingana na ripoti ya
Shirika la Afya Duniani(WHO)
ya mwaka 2010, vifo vinavyotokana na malaria vimepungua Barani Afrika na
hii ni kwa
sababu ya juhudi za makusudi
za kutokomeza malaria, juhudi hizi zimetekelezwa
katika nchi mbalimbali kwa kushirikiana na wenza kimataifa.
Katika
kikao cha leo
nchi nne zimefuzu na kupokea
Tuzo ya Kwanza ya Ubora na
Umakini katika Juhudi za Kupambana
na Malaria zikiwemo Tanzania,
Guinea, Kenya na Uganda. Juhudi zilizofanywa na nchi hizi ni
pamoja na kukuza uhusiano na kuharakisha upatikanaji wa fedha, kudhibiti na kukuza matumizi
ya kinga ya malaria, mfano ikiwemo matumizi ya vyandarua, kufuta
na kusitisha utengenezaji, usambazaji na matumizi ya
dawa aina ya Artemisinin, kuondosha kodi na kuunga mkono
utengenezaji na uzalishaji wa dawa
za malaria Barani Afrika. Rais Kikwete amepokea
tuzo hiyo katika kikao cha leo na kushuhudiwa
na nchi wanachama
wakiwemo pia Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mmataifa Ban Ki Moon, mwenyeji wa Mkutano
wa Viongozi wa Afrika wanaohudhuria
kikao jijini Addis Ababa Waziri Mkuu Meles
Zenawi viongozi wa mashirika ya
kimataifa na nchi rafiki.
Katika
kikao cha leo
Rais wa Liberia Ellen
Johnson Sirleaf amechaguliwa
kuwa Makamu Mwenyekiti wa ALMA. Rais Kikwete yuko Addis Ababa kuhudhuria kikao cha Viongozi wa
Afrika kinachotazamiwa kumalizika leo jioni. Rais anatarajiwa kurejea nyumbani kesho tarehe 1 Februari, 2011.
Mwisho.
Imetolewa
na Primi
Kibanga,
ADDIS ABABA.
Ethiopia.
31
Januari, 2011