UNITED REPUBLIC OF
TANZANIA
DIRECTORATE OF
PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S
OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX
9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Iran imetoa matrekta madogo aina ya power tiller 100 kwa Serikali
ya Muungano wa Tanzania katika kusaidia kuinua na kuimarisha kilimo
nchini na hasa kuunga mkono
malengo ya Mpango wa Kilimo
Kwanza.
Mchango huo mkubwa wa
kusaidia kuinua na kuboresha kilimo
cha Tanzania umeelezwa na Balozi wa Iran katika Tanzania, Mheshimiwa Mohsen Movahhedi Ghumi kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete wakati alikutana na kufanya mazungumzo
na balozi huyo.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo, Alhamisi, Oktoba 13, 2011, Ikulu, Dar es Salaam, Balozi huyo amemweleza
Rais Kikwete kuwa matreka hayo
madogo yenye thamani ya dola
za Marekani 600,000 yamenunuliwa kutokana na sehemu ya
msaada wa maendeleo wa Iran kwa Tanzania.
Mwaka jana, Tanzania na
Iran zilitiliana saini makubaliano ambako Iran iliahidi kuipatia Tanzania msaada wa maendeleo
wa dola za
Marekani milioni 1.2.
Sehemu ya msaada huo
ndiyo imetumika kununulia matekta hayo na kiasi kinachobakia cha dola za Marekani
600,000 kitatumika kujenga kliniki ya kisasa
mjini Dar es Salaam kwa ajili ya
kuongeza huduma za afya kwa
wakazi wa jiji hilo.
Katika makubaliano hayo hayo, Iran ilikubali kutoka msaada wa dola za
Marekani milioni moja kwa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar ambako kati ya hizo
kiasi kitatumika kununulia matreka madogo 50 kwa ajili
ya kuendeleza kilimo Visiwani na kiasi kinachobakia
kitatumika kupata boti kwa ajili
ya kuimarisha shughuli za uvuvi
Tanzania Visiwani.
Matreka hayo yote ambayo
yanatolewa kwa
Tanzania yatakabidhiwa rasmi
karibuni na kiongozi mmoja mwandamizi wa Serikali
ya Iran ambaye atatembelea Tanzania kwa muda wa siku
mbili.
Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete amemshukuru
Balozi wa
Iran kwa msaada huo akisema kuwa
matreka hayo yatakuwa mchango mkubwa katika kufanikisha
Mpango wa Kilimo Kwanza.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
13
Oktoba, 2011