DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 E-mail: press@ikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENTS OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Na Mwandishi Maalum, Mwanza
RAIS Jakaya
Mrisho Kikwete ametaja misingi mikuu mitatu iliyowekwa
na Hayati
Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere katika kulijenga taifa la
Aidha, Rais
Kikwete amewashangaa Watanzania ambao wanabeza uhuru wa
Ameitaja misingi
hiyo mikuu kuwa ni uhuru, umoja wa
taifa la
Rais Kikwete
ameyasema hayo mjini Mwanza jioni
ya jana,
Jumamosi, Oktoba 3, 2009 alipozungumza na vijana wa CCM ambao
wanaondoka mjini Mwanza leo kwenda
Butiama, Mkoani Mara, kwa Matembezi Maalum
ya kumuezi Mwalimu kwenye kumbukumbu ya miaka
10 tokea kufariki kwake, Oktoba 14, 1999.
Vijana 166 kutoka
mikoa yote ya
Kauli mbiu
ya Matembezi hayo ni
Uhuru na Kazi na miongoni
mwa mambo ambayo vijana hao watafanya
njiani ni kukarabati Shule ya Msingi ya
Mwisenge ambako Mwalimu Nyerere alipata elimu yake
ya msingi.
Rais Kikwete
amesema kuwa urithi mkuu ambao
Mwalimu aliwaachia Watanzania ni
misingi hiyo mikuu ambayo imeendelea
kulifanya Taifa la
Aidha, Rais
Kikwete amesema kuwa kila taifa
duniani linalo waasisi wake ambao wanastahili kuendelea kukumbukwa siyo tu kwa uasisi pekee, lakini
kwa mambo ambayo waliyasimamia, waliyaamini na waliyajenga.
Wamarekani
wale wanaye George Washington
sisi
tunaye Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
na kila nchi ina mwasisi
wake ambaye anakumbukwa kwa aliyoyasimamia, amesema Mwalimu na kuongeza:
La kwanza la kumkumbuka Mwalimu ni uhuru
wa nchi yetu.
Huyu alikuwa ni
kiongozi aliyeambiwa achague kati ya
siasa ama kazi ya ualimu
huyu mzee wetu akachagua siasa na utumishi
wa umma bila
hata kujua atakula nini.
Akachagua kupigania uhuru wa nchi
yetu.
Rais Kikwete
amesema kuwa uhuru siyo mipaka
bali ni
heshima ya nchi na ndiyo
maana
Amesisitiza: Mwaka
1978, yule msanii na profesa
wa historia na jiografia, Idi
Amin alivamia nchi yetu
. na
sisi tukamfurumusha ili kulinda uhuru
wetu na wako
wenzetu ambao walipoteza maisha
Rais Kikwete
pia amewashangaa wale wote ambao wanafurahia
wakati heshima ya
Kuhusu umoja
wa taifa,
Rais Kikwete amesema kuwa Mwalimu
alihakikisha kuwa uhuru wa nchi
unazaa umoja ili nchi iwe
moja na isigawanyike
vipande vipande kwa sababu yoyote
ile.
Aliondoa
viashiria vyote vya kuvunja umoja
wa taifa tokea mwanzo kabisa. Aliondoa
uchifu ili
kuondoa nguvu za ukabila. Alitambua
hatari ya dini na akataifisha shule zote za dini
ili vijana wetu waelimishwe na kulelewa
Rais Kikwete
amesema kuwa hata kabla ya
uhuru, Mwalimu alitambua ili uhuru
na umoja viweze kudumishwa ni lazima wananchi
wake wapate maisha bora na ndiyo
maana akawatambua maadui wakuu watatu
ujinga, maradhi na umasikini- na
njia za kukabiliana
na maadui hao.
Wapo
watu wanaobeza kuwa hii sera ya
maisha bora imeletwa na
akina Kikwete. Sisi tumeendeleza sera ile ile ambayo
taifa hili limekuwa linatekeleza tokea uhuru wetu
na wala
kazi hii haitaishia kwangu mimi, hata wale viongozi watakaonifuata wataendeleza sera hii kwa sababu kazi
ya kujenga maisha bora kwa
wananchi haihishi, haina kikomo.
Amesisitiza Rais
Kikwete: Tunapojenga shule tunapambana na ujinga, tunapojenga
chuo kikuu kipya pale Dodoma tunapambana na ujinga
tunapopanua
huduma za afya tunapambana na maradhi, tunapoelekeza
nguvu zetu kupambana na ukimwi
tunapambana na maradhi
tunapojenga barabara tunapambana na umasikini, tunapoanzisha
Kilimo Kwanza tunapambana na umasikini