DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

 

 

PRESIDENT’S OFFICE,

      THE STATE HOUSE,

       P.O. BOX 9120,  

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

 

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Sirlius B.M. Gwazidoro Matupa kuwa Msaidizi wa Rais - Masuala ya Sheria.

 

Taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi, Novemba 5, 2009, Ikulu, mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Philemon Luhanjo, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Jumanne, wiki hii, Novemba 3, 2009.

 

Bwana Sirlius Matupa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana George Msaju, ambaye majuzi aliteuliwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

 

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Matupa alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.

 

Imetolewa na:

 

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

 

05 Novemba, 2009