UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE
STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR
ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia salamu za rambirambi Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba
Makinda (MB.,) kutokana na kifo
cha Mhe. Jeremia Solomon Sumari, aliyekuwa Mbunge wa
Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi
ya CCM na aliyepata kuwa Naibu Waziri, kilichotokea
usiku wa kuamkia leo tarehe
19 Januari, 2012 katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na
taarifa za kifo cha Mheshimiwa Jeremia Solomon Sumari kwani alikuwa kiongozi
aliyewatumikia vema wananchi wa Jimbo
lake la Uchaguzi la Arumeru
Mashariki na Taifa kwa ujumla
katika wadhfa wake wa Waziri kwa
umahiri na uhodari mkubwa”, amesema Rais Kikwete
katika salamu zake.
Rais Kikwete amesema kutokana na
kifo chake, wananchi wa Arumeru
Mashariki wamepoteza kiongozi wa kutegemewa
sana huku Taifa likiachwa na pengo kubwa
ambalo si rahisi kuzibika ikizingatiwa kwamba alikuwa kiongozi katika Wizara ambayo
ni mhimili muhimu kwa maendeleo
ya nchi yetu.
“Kwa dhati ya
moyo wangu, natuma salamu za
rambirambi na
pole nyingi kwa familia ya Marehemu
Jeremia Sumari kwa kumpoteza kiongozi
na mhimili madhubuti wa familia. Ninawahakikishia kwamba nipo pamoja
nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa, na namuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema
aipumzishe roho ya Marehemu Jeremia
Solomon Sumari mahali pema peponi, Amina”,
ameongeza kusema Rais Kikwete.
Ameiomba familia ya Marehemu
kuwa na
moyo wa uvumilivu
na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa
wao kwa kutambua
kuwa yote ni mapenzi yake
Mola.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
19 Januari,
2012