UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Shirika
la Makapuchini nchini
Tanzania, Padre Wolfgan Peter, kuomboleza vifo vya mapadre wanne
wa shirika hilo waliopoteza
maisha yao katika ajali ya
gari jana,
Jumanne, Novemba 22, 2011 eneo la Ruvu kwa
Zoka, Bagamoyo,
mkoa wa Pwani.
Katika salamu hizo, Mheshimiwa Rais Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na kuhuzunishwa
na vifo vya
mapadre hao. “Nimepokea kwa
masikitiko na huzuni nyingi habari
za vifo vya
mapadre wa Shirika lako la Makapuchini katika ajali ya gari.
Napenda kukutumia wewe binafsi salamu za rambirambi na
kupitia kwako kwa waumini wote
wa shirika lako.”
Ameongeza Rais Kikwete katika salamu zake:
“Napenda kukuhakishia kuwa Serikali yangu
na mimi
binafsi tuko nanyi katika wakati
huu wa huzuni.
Msiba wenu ni msimba
wetu. Namwomba Mwenyezi Mungu
aziweke pema peponi roho za
marehemu. Amen.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
DODOMA.
23 Novemba, 2011