UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
jioni ya leo, Jumatatu, Januari 9, 2012, amekutana na kufanya mazungumzo
na mjumbe maalum wa Rais
wa Gambia, Mheshimiwa Yahya A. Jammeh.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, mjumbe huyo maalum, Mheshimiwa
Lamin Kaba ambaye pia ni Waziri wa Uvuvi, Maliasili
na Masuala ya Bunge amemkabidhi Rais Kikwete ujumbe
maalum kutoka kwa Rais Jammeh.
Katika mazungumzo yao,
Rais Kikwete na Mheshimiwa Kaba
wamezungumzia masuala yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Gambia na pia
masuala ya Afrika na ya
kimataifa.
Mjumbe huyo maalum anatarajiwa
kuondoka nchini kesho kwenda Nairobi, Kenya ambako anatarajiwa kukutana na
viongozi wa nchi hiyo.
Imetolewa na:
Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
09
Januari, 2012