UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ameielezea Uingereza kama mshirika kakati
(strategic partner) katika maendeleo
ya Tanzania kutokana na miaka 50 ya
ushirikiano na misaada ya maendeleo
na ya kiufundi
kutoka kwa nchi hiyo.
Aidha, Rais Kikwete ametaka
nchi zote mbili, Tanzania na Uingereza, kuongeza jitihada za kuvutia
uwekezaji zaidi katika Tanzania kutoka Uingereza ambao thamani yake kwa
sasa inafikia dola za Marekani
bilioni 1.8 (sawa na sh. bilioni 3060).
Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa jana, Jumatatu, Novemba 8, 2011, Ikulu, Dar es Salaam, wakati wa Chakula
cha Kitaifa alichomwandalia
Mtoto wa Malkia wa Uingereza,
Prince Charles ambaye anatembelea
Tanzania na mkewe, Mama
Camilla. Prince Charles na Mama Camilla wako kwenye ziara
ya siku tatu
nchini Tanzania.
Rais Kikwete amesema kuwa ziara ya
Prince Charles imetoa nafasi
kwa Tanzania kuwashukuru wananchi wa Uingereza kwa
misaada yao mikubwa ambayo kwa miongo mitano
iliyopita wametoa kuchangia maendeleo ya Tanzania.
“Misaada ya Serikali ya
Malkia na
wananchi wa Uingereza imekuwa muhimu sana katika
jitihada zetu za kujikomboa kutoka
umasikini na kuelekea katika maisha bora zaidi. Katika miaka 50 iliyopita mumekuwa nasi katika
nyakati za raha na nyakati za shida
na wananchi wa Tanzania wamenufaika sana kutoka na
misaada ya maendeleo na ya
ufundi kutoka Uingereza,” Rais Kikwete amemwambia Prince Charles
na ujumbe wake.
Ameongeza Rais Kikwete katika
hotuba yake fupi: “Misaada muliyotupa imesaidia sana kuboresha
kiwango cha maisha ya Watanzania wengi.
Imeleta tofauti kubwa katika
maisha ya wananchi wetu.”
Rais kikwete amesema kuwa mbali na Uingereza kuwa chanzo kikubwa
zaidi cha misaada ya maendeleo na
ya kiufundi, nchi hiyo pia
imekuwa chimbuko kubwa zaidi la mitaji inayoingia katika uchumi wa
Tanzania.
“Ninayo furaha kusema kuwa
mbali na
kuwa chanzo kikubwa zaidi cha misaada ya maendeleo
na ufundi, Uingereza pia imekuwa
nchi inayoongozwa kwa kuleta uwekezaji
na mitaji katika nchi yetu.
Kwa sasa uwekezaji kutoka Uingereza unafikia dola za
Marekani bilioni 1.8.
Lakini utakubaliana nami kuwa kwamba tunaweza
kufanya vizuri zaidi kuliko tulipo
na lazima
tulenge kufanya vizuri zaidi. Kwa hakika, Uingereza
ni mshirika kakati wa maendeleo
yetu,” Rais Kikwete amesema.
Prince Charles yuko
nchini kwa
mwaliko wa Serikali kwa ajili
ya kushiriki katika sherehe za miaka 50 ya
Uhuru wa Tanzania Bara. Alikuwa Prince Philip (Duke of Edinburgh), baba yake Prince Charles, ambaye alimkabidhi funguo za Uhuru wa Tanzania Bara Mwalimu
Julius Nyerere, waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru na Baba wa Taifa
la Tanzania.
Imetolewa na:
Mkurugenzi wa Mawasiliano
ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
08
Novemba, 2008