UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Desemba
30, 2011, amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu
na Naibu Katibu Mkuu na
pia amefanya uhamisho wa Katibu
Mkuu na Naibu
Katibu Mkuu kuanzia jana, Alhamisi,
Desemba 29, 2011.
Taarifa iliyotolewa na
Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Phillemon Luhanjo, inasema kuwa Bwana Fanuel E. Mbonde, Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Ikulu, anahamishiwa Wizara ya Katiba na
Sheria, na Bwana Alphayo Kidata, Naibu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Ikulu, anahamishiwa
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala
za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI).
Aidha, taarifa hiyo inasema
kuwa Bwana Eliakim C. Maswi, ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu,
Wizara ya Nishati na
Madini. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Maswi alikuwa Naibu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kwa
sasa anakaimu nafasi ya Katibu
Mkuu, Nishati na Madini.
Mheshimiwa Rais Kikwete pia
amemteua Bwana Peter Ilomo,
Mratibu Mkuu wa Sera na
Mipango, Ofisi ya Rais, Ikulu,
kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais, Ikulu.
Naye
Bibi Susan Paul Mlawi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Ikulu. Kabla ya uteuzi
huu, Bibi Mlawi alikuwa Msaidizi
wa Katibu
wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Under Secretary) Kamati ya Katiba
na Bunge ya Baraza la Mawaziri.
Taarifa ya Bwana Luhanjo inamalizia kwa
kusema kuwa mabwana Maswi na
Ilomo pamoja na Bibi Mlawi
wataapishwa Jumatatu, Januari 2, 2012, saa nne asubuhi, Ikulu,
Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
30
Desemba, 2011