UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Balozi Ombeni Yohana Sefue
kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Balozi Sefue anachukua nafasi inayoachwa wazi na
Bwana Phillemon Luhanjo ambaye anahitimisha mkataba wake wa utumishi wa umma
kesho, Jumamosi, Desemba 31, 2011.
Kabla ya uteuzi wake, Balozi Sefue alikuwa
Balozi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa, New York, Marekani.
Kabla ya hapo, Balozi
Sefue alikuwa Balozi wa
Tanzania nchini Marekani na kabla ya
hapo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada tokea Oktoba 2005.
Balozi Sefue ataapishwa kesho, Jumamosi, Desemba 31, 2011 saa nne asubuhi,
Ikulu, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
30
Desemba, 2011