UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
na ujumbe wa Serikali yake
leo, Jumapili, Novemba 27, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo
na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA).
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, yamefanyika katika mazingira ya urafiki
na ujumbe
wa CHADEMA umewasilisha mapendekezo yake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba
Mpya ya Tanzania. Serikali imepokea mapendekezo
hayo.
Hata hivyo, pande zote
mbili zimekubaliana kukutana tena asubuhi
ya kesho, Jumatatu, Novemba 28, 2011, ili kuipa
nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo hayo.
Lakini pande hizo mbili
zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa
ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka
50 iliyopita kwa sababu ni Katiba
ya sasa iliyoliwezesha
Taifa la Tanzania kuwa na amani,
utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata
mpaka sasa.
Pia pande zote mbili
zimekubaliana kuhusu umuhimu wa
kutunga Katiba Mpya kama Mheshimiwa
Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu
zake za mwaka
mpya Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba ambayo italiongoza
Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo.
Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Rais aliwahakikishia wajumbe hao wa
CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama
hicho, Mheshimiwa Freeman Mbowe kuwa ni
dhamira yake na ya Serikali
yake kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba mpya.
Katika mkutano huo, pande
zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu
sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa
Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya
kulinda na kudumisha tunu za taifa za
amani, utulivu na umoja wa
kitaifa.
Aidha, pande zote mbili
zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe
kwa kuzingatia
misingi ya mambo mengine muhimu kwa taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya
uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi
ya udini na ukabila ama
kutugawa kwa misingi ya maeneo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27
Novemba, 2011