UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumanne, Novemba 15, 2011, amepokea hati za utambulisho
za mabalozi wapya watakaoziwakilisha nchi za Uswisi
na Ufaransa katika Tanzania.
Katika sherehe fupi iliyofanyika
Ikulu, Dar es Salaam, Rais Kikwete amepokea
hati za utambulisho
kutoka kwa
Balozi mpya wa Uswisi, Mheshimiwa
Oliver Chave, na kutoka kwa Balozi
mpya wa Ufaransa,
Mheshimiwa Marcel Escure.
Katika mazungumzo yaliyofuatia baada ya kuwa
amepokea hati za Mheshimiwa Chave,
Rais Kikwete ameishukuru Uswisi kwa misaada
yake ya maendeleo
kwa Tanzania hasa katika nyanja ya
afya. “Misaada
yenu katika eneo hili, Mheshimiwa
Balozi, imeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya
Watanzania. Tunawashukuru sana
kwa misaada hiyo.”
Rais Kikwete amemwelezea Balozi Chave kuhusu
mipango ya Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi kupitia
sekta ya afya na hasa juhudi za
Serikali kuhakikisha kuwa inajenga zahanati
kila kijijiji na kituo cha afya
kila kata ili kupunguza umbali ambao wananchi wanatembea kutafuta huduma za afya.
Balozi Chave amemwambia Rais Kikwete kuwa
Uswisi na
wananchi wa nchi hiyo wanaipongeza
Tanzania na kuitakia heri katika kuadhimisha
miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Katika mazungumzo na
Balozi Escure, Rais Kikwete ameishukuru
Ufaransa kwa misaada yake katika
maeneo mbalimbali hasa ya maji
na utalii ambako nchi hiyo
imesaidia ujenzi wa chuo kipya
cha kufundisha wataalam wa utalii nchini
ambacho ujenzi wake umekamilika mjini Dar es Salaam.
“Tunaishukuru Ufaransa kwa kutujengea chuo hiki. Tunafanya vizuri sana katika
sekta ya utalii lakini hatukuwa
na chuo cha kuweza kutufundishia wataalam wetu katika
eneo hili. Tunashukuru kwamba Ufaransa imesaidia kujengwa kwa chuo
hicho,” amesema Rais na kuongeza:
“Tunashukuru
pia kwa
kusaidia miradi ya maji katika
miji yetu midogo. Wakati mwingine ni
rahisi kuboresha miundombinu katika miji mikubwa na
kuisahau ile midogo lakini tunashukuru
kwa msaada wenu katika eneo
hilo.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
15
Novemba, 2011