UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116539 E-mail: press@ikulu.go.tz Website: www.mawasilianoikulu.go.tz Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amesema kuwa Serikali inakamilisha mipango ya kuanzisha
upya utaratibu wa vijana kujiunga
na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa
sheria kama ilivyokuwa zamani.
Aidha, Rais Kikwete amesema
kuwa Tanzania iko tayari kutoa uzoefu
wake wa jinsi
ya kuendesha JKT kwa Zimbabwe ambayo nayo inaangalia jinsi ya kuanzisha
jeshi kama hilo kwa ajili
ya vijana.
Rais Kikwete ameyasema hayo, leo, Jumamosi,
Novemba 5, 2011, Ikulu, Dar
es Salaam, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi ya Zimbabwe Jenerali Constantine G. Chiwenga ambaye alikuwa katika ziara ya
Tanzania.
Katika mazungumzo hayo, Jenerali Chiwenga amemweleza Rais Kikwete kuhusu hali ya kisiasa
na kiuchumi
katika Zimbabwe ikiwa ni pamoja na
mchakato wa maandalizi ya katiba
mpya ya nchi
hiyo ambayo inafungua mlango wa kufanyika kwa
uchaguzi mkuu mwingine nchini humo.
Jenerali Chiwenga pia ametumia
mazungumzo hayo na Rais Kikwete kuishukuru tena Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika mapambano ya ukombozi wa
Zimbabwe.
Rais Kikwete ameitakia Zimbabwe na wananchi
wake mafanikio katika mchakato wa mageuzi
ya kisiasa na kiuchumi na
kusisitiza kuwa Tanzania iko tayari kutoa
mchango wowote ambao Serikali na wananchi wa
Zimbabwe watautaka kutoka kwa Tanzania na Watanzania.
“Tuko nanyi. Tanzania iko na wananchi
wa Zimbabwe. Huu ni uhusiano
wa kihistoria ulioanzia kwenye makambi ya wapigania
uhuru ya Kongwa na Nachingwea
hadi kwenye misitu ya Mozambique mpaka ndani ya
Zimbabwe yenyewe,” amesema Rais Kikwete na
kuongeza. Ni uhusiano uliojengeka kwa
damu ya Watanzania
na Wazimbabwe,” Rais Kikwete amemwambia
Jenerali huyo katika mazungumzo ambayo pia yamehudhuriwa
na Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
05
Novemba, 2011