UNITED
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone:255-22-2114512, 2116898 E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE, THE STATE HOUSE, P.O. BOX 9120, DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Alhamisi, Desemba Mosi, 2011, amekutana na kufanya
mazungumzo na Rais Mstaafu wa
Marekani Mheshimiwa George
W Bush ambaye yuko katika ziara ya
siku sita nchini Tanzania.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, viongozi hao wamezungumzia jinsi Taasisi ya
Mheshimiwa Bush ya George W
Bush Institute for Global Health inavyoweza kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na changamoto kubwa
za sekta ya afya na
hasa magonjwa ya saratani.
Mheshimiwa Bush ambaye anafuatana na mkewe
Mama Laura Bush amemweleza Rais
Kikwete mipango ya taasisi yake
katika kupambana na ugonjwa wa
kansa ikiwa ni pamoja na
jitihada za kupima, kuzuia na chanjo.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa
pia na Mama Salma Kikwete, Rais Kikwete
ametumia nafasi hiyo kumweleza Mheshimiwa Bush jitihada za serikali yake
katika kupambana na magonjwa yanayoua
watu wengi ikiwamo malaria, ukimwi na saratani, magonjwa
ambayo mapambano yake Mheshimiwa Bush alichangia sana kifedha alipokuwa madarakani.
Rais Kikwete pia ametumia
nafasi hiyo kumweleza Mheshimiwa Bush kuhusu mipango mingine ya maendeleo
inayosaidiwa na
Marekani ikiwa ni pamoja na
mpango mkubwa wa ujenzi wa
miundombinu chini ya Mpango wa
MCC.
Rais Bush na familia
yake wako katika ziara ya
Afrika na mbali ya Tanzania wanatembelea pia Ethiopia na Zambia.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
01
Desemba, 2011